Showing posts with label Ngwair. Show all posts
Showing posts with label Ngwair. Show all posts

Sunday, September 15, 2013

Mama Ngwair Amtetea Mwana Fa

Mama wa MwanaHip Hop aliyewahi kuaminika kuwa bingwa wa mitindo huru, Albert Mangwea aliyefariki mwezi Mei mwaka huu, Denisia Costantine Mangwea ameibuka na kumtetea mwanamuziki wa kizazi kipya Hamis Mwin’juma ambaye anatuhumiwa kuahidi pesa kwa mama huyo na kuingia mitini.
Sakata hilo ambalo limekuwa likiripotiwa tangu mwishoni mwa wiki iliyopita, linatokana na kitendo cha mwanamuziki huyo (MwanaFA) ambaye aliwahi kuahirisha onesho lake, baada ya kifo cha msanii mwenzake (Albert Mangwea), kutokuweka hadharani....Read More

Tuesday, June 4, 2013

Baadhi ya Post za Wasanii na Mashabiki Toka Kifo cha Ngwair













UPDATES: Mwili wa Ngwair Wawasili Muhimbili

                                                                          Picha kwa hisani ya DjChoka

PHOTOS: Mwili wa Albert Mangwea Wawasili, Mashabiki washindwa kuamini kama ni kweli

Baadhi ya Mashabiki wakiwa Airport kuupokea mwili wa marehemu Ngwair
 


Professor Jay akifanya Interview, kulia ni Producer Lamar



Hapa ni safari ya kuelekea ilipoanza

Lamar na Jay Moe




IKIWA ni leo ndiyo mwili wa Marehemu wa Albert Mangwea umewasili nchini, maelfu ya mashabiki wamejitokeza kuupokea mwili wa msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya.
Katika mapokezi hayo watu walikuwa wengi zaidi kiasi cha mashabiki wake hao kupingana na kauli ya polisi waliotaka gari lililobeba mwili wa marehemu Ngwair kuendeshwa lakini wao walitaka kulisukumu gari hilo mpaka hospitali ya Taifa Muhimbili na wengine wakitaka jeneza litolewe ili walibebe kwa mikono mpaka Muhimbili.
Mashabiki hao waliojipanga pembezoni mwa barabara kushuhudia mwili wa mpendwa wao Ngwair, licha ya wengi wao kushuhudia gari lililobeba jeneza lenye mwili wa Ngwair lakini miongoni mwao walionekana bado hawaamini kama kweli msanii huyo amefariki.

Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, Aminnnnn!!!

Wednesday, May 29, 2013

R.I.P ALBERT MANGWEA a.k.a NGWAIR

Ni moja kati ya wasanii wabongo aliyekuwa akifanya poa sana, nyota ilionekana tangu miaka ya 2000 alipoatoa nyimbo yake ya Ghetto langu ambayo iliwabamba fans wa muziki wa kizazi kipya.
Jamaa ambaye alikuwa amejibatiza a.k.a kibao.........a.k.a Cowboy, Cowweezy, Mtoto wa Jakaya, King wa freestyle, Jembe, NGE, A.K.A mimi na nyingine kibao. Pengo lake halitazibika alikuwa na kipaji cha aina yake...Rest in Peace Albert Mangwea
 

Saturday, February 9, 2013

Quick Rocka Kuangusha Mzigo Mpya 'My Baby' Ft Ngwair... Kama wewe ni Shabiki wake inakuhusu

 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Quick Rocka amesema anatarajian kuachia ngoma yake mpya ambayo atakuwa amemshirikisha mwana Chamber Squad ‘Ngwair’.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, hitmaker wa Katika, amewataka fans wa muziki wa kizazi kipya kukaa tayari kwani itakuwa ni bonge ya ngoma inayofanyika katika studio za A.M Records chini ya Producer Manecky, jina la ngoma hiyo ni My Baby.


Wednesday, January 23, 2013

Tuesday, January 15, 2013

NEW TRACK: Naj Ft Ngwair - NAJ