Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Monday, August 15, 2016

HAWA NDO WANAHIP HOP ANAOWAKUBALI CHINDO MAN


Msanii wa hip hop tokea Arusha Chindo amewataja wana hip hop anaowakubali zaidi Tanzania.

Akitambulisha video yake mpya ya Torati ya mtaa kwenye kipindi cha Friday night Live Chindo amemtaja Hashimu Dogo kama namba moja,Fid Q akifuatiwa na JCB kama wana hip hop anaowakubali kwa Tanzania na Afrika.

Kwa upande wa mbele Chindo amewataja Nas Escobar, Jay z, J Cole, Kendrick Lamar na Meek Mill kama wana hip hop anaowakubali zaidi.

Thursday, August 4, 2016

MSANII UDE UDE AFARIKI DUNIA TANGA


Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Fleva,Hamid Hafidhi maarufu kama Ude Ude na rafiki yake Iku wamefariki dunia wakiwa mkoani Tanga.
Marehemu Ude Ude na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo enzi za uhai wao
Marehemu Ude Ude na rafiki yake Iqu Junior ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo enzi za uhai wao
Marehemu Ude Ude alijipatia umaarufu kwenye muziki wa bongo fleva kwa umahiri wake wa kuwatungia nyimbo wasanii ambapo nyimbo alizozitunga ni pamoja naWangu na Yahaya za Lady Jay dee,Ballin and Chillin ya Sammisago.
Ude Ude na Iqu Junior wanadaiwa kuuawa katika tukio la ujambazi lilitokea mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wawili hao walikuwa miongoni mwa majambazi wanne waliokuwa na gari aina ya Toyota Probox waliokurupushwa na polisi katika jaribio la kuiba vifaa vya magari ya halmashauri.

Tukio hilo lilitokea jana saa mbili asubuhi walipokutwa wakivunja gari la mwalimu wa shule ya sekondari, Maweni aliyejulikana kwa jina la Dominica Tarimo.

Wananchi wakiwa na piki piki na magari pia waliungana na polisi kuwafukuza watu hao na kuwashambulia. 
Polisi hao wamedai watu hao walijihami na silaha zenye ncha kali ili kujiokoa na wawili kupiga risasi huku wawili wakitokomea kwenye msitu ulio jirani na kiwanda cha saruji cha Sungura.
Hapa chini nimekuwekea taarifa hiyo ya gazeti la Mwananchi.
10d2cf02-3ce6-489c-ae4a-e05f0114530d.jpg
R.I.P Rafiki Zetu, Roho za Marehemu zilale mahali pema peponi Amen.

Tuesday, August 2, 2016

BABU TALE ALALA POLISI, AFIKISHWA MAHAKAMA KUU DAR

MENEJA wa msanii Diamond Platnumz, Hamis Taletale “Babu Tale” amefikishwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akitokea kituo cha polisi ambako alilala jana baada ya mahakama kutoa amri ya kukamatwa kutokana na kutotii amri iliyomtaka amlipe Sheikh Hamis Mbonde Sh milioni 250.

Babu Tale ambaye alifika mahakamani hapo mapema kabla ya kuitwa kwa kesi hiyo iliyoanza saa 10:40  asubuhi, miguuni alikuwa amevalia kandambili huku akisindikizwa na Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe,  Said Fella pamoja na msanii chipukizi wa Bongo fleva kutoka lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond.

Meneja huyo anatakiwa alipe fedha hizo kutokana na kuvunja mkataba kati yake na Shekhe Mbonde, kwa  kuuza na kusambaza  nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya Shekhe huyo, jambo ambalo ni kinyume na haki miliki.

Wakili wa upande wa mdai, Mwesiga...Isome zaidi kesho katika Gazeti la HabariLeo

Saturday, July 30, 2016

RICK ROSS AMSAINI OMBAOMBA KWENYE LEBO YAKE

isa-2
Rapper Rick Ross na bosi wa Maybach Music Group, amemsaini rapper asiyekuwa na makazi aliyekutana naye barabarani na kuanza kuchana mbele yake ili kupata nafasi ya kuwa kwenye lebo yake.

Isa Muhammad ni rapper asiyekuwa na makazi ya kuishi na kwao ni California ambaye amekuwa na bahati ya mtende kwa kulifurahisha sikio la Rozay na kuwa msanii mpya wa MMG.


Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Rozay amesema hakutegemea kumsaini msanii huyo ila uwezo na moyo wake ulimfanya iwe rahisi kumkubali.
isa-muhammad

MUBENGA AFICHUA KISA CHA KUACHANA NA OMMY DIMPOZ (PKP)

ommy-dimpoz-na-Meneja-wake-MubengamubaAliyekuwa meneja wa msanii wa muziki Ommy Dimpoz, Mubenga, amekanusha taarifa ambazo zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa kilicho muachanisha na Ommy Dimpoz ni kudhurumiana pesa.

Hapo awali Mubenga alisema aliamua kuachana na Ommy Dimpoz ili na yeye afanye mambo yake bifansi pamoja na kuanzisha label yake mpya ya muziki itayokuwa inasimamia wasanii.

“Kiukweli ni kwamba hakuna tatizo, ni mambo ya kazi PKP ni kama nyumbani tu, nimeamua kuhama nyumbani na kwenda kuanzisha maisha yangu,” Mubenga alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Hakuna kudhurumiana, hiyo stori ndo naisikia kwako, hakuna kitu kama hicho, na mimi sina tatizo na Ommy Dimpoz,”

Mubenga kwa sasa ameanzisha label yake mpya ‘Bengaz Entertainment’ ambayo itaanza kusaini wasanii wa muziki hivi karibuni.
Source: Bongo5.com 

MR T-TOUCH ATOA SHARTI LA KUFANYA KAZI NA NAY WA MITEGO

http://www.perfect255.com/wp-content/uploads/2016/07/img_BH4A6-1Dp5k.jpgKama ni mfuatiliaji wa muziki wa Bongo Fleva utagundua kuwa hits nyingi za msanii Nay wa Mitego ni nyimbo ambazo zimetengenezwa na Producer Mr T-Touch.

Wawili ambao wiki chache zilizopita walikua wakifanya kazi pamoja katika studio za Free Nation studio ambayo Nay wa Mitego aliamua kumzawadia producer huyo kwa kile kikubwa ambacho Nay aliamini amefanyiwa na Producer huyo.

Siku chache zilizopita zilizuka taarifa kuwa Mr T-Touch hayupo tena katika studio za Free Nation kwa kile kilichoaminiwa kuwa kuna mifarakano ambayo imetokea baina ya wawili hao. Nay wa Mitego alitafutwa na E.News ya EATV na kuulizwa kuhusu hili na kudai kuwa yeye hana tatizo kabisa na Mr T anakiheshimu kile ambacho amemfanyia..

 Leo Clouds E ya Clouds TV imemtafuta Mr T-Touch na kupiga nae story kuhusu issue hiyo na haya ndio yalikua majibu ya Mr T

''Nimeondoka kwa nay kwasababu nataka kuipa thamani kazi yangu, nitafanya kazi  na Nay endapo atanilipa nitakavyo. Me nafanya kazi na wasanii wengi na wananilipa pesa nzuri, mfano mzuri Billnass me ananilipa zaidi yaMilioni kwa ngoma moja''

Mr T-Touch aliweka wazi kuhusu kufungua studio yake binafsi na kudai kwamba ametengeneza studio kwa gharama kubwa ila hawezi kupandisha kiwango cha bei ya kurekodi ngoma kwasababu anataka studio yake iweze kufanya kazi hata na ma underground hivyo kiwango ni kile kile cha mwanzo ambacho hata msanii mchanga anaweza kukimudu.

Friday, July 8, 2016

BARAKA DA PRINCE AJIUNGA NA ROCKSTAR400

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEj1AUXxlF-JvAnqA6xXDhlNSRdUNf6p4Bj49ry7C2g3SBsWM_DWcAG7I_i9lzTcDTzkT1Bij-PVq0KtYa3CwJ4W1CwOfqix0aWjIV3gwgfz240K9SJ3xTs5MLk1jlw29Ddelk9eTQqmbw8/s1600/wp-1467956003926.jpg

Hitmaker wa Siwezi, Barakah Da Prince amesainishwa mkataba wa usimamizi na kampuni ya Rockastar4000.

Ameungana na Alikiba na Lady Jaydee kuwa msanii wa tatu kuwa chini ya uongozi huo. Na kwa sasa muimbaji huyo atakuwa akijulikana kama ‘Barakah The Prince.’

Kwenye maelezo yake, CEO na mwanzilishi wa label hiyo, Jandre Louw amedai kufurahishwa kumsaini muimbaji huyo wa Mwanza na kumwelezea kama mwenye kipaji cha hali ya juu.

Monday, July 4, 2016

HIKI NDICHO YOUNG DEE ALICHOWAJIBU MTU CHEE

13531968_1101664066571243_1094846367_nRapper Young Dee amesema suala la yeye kuwapigia magoti Stamina na Country Boy ili arudi kwenye kundi la Mtu Chee ‘halimake sense.’

Stamina alidai kuwa kutoka kwa Young Dee kwenye kundi hilo kulitokana na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.

“Suala la mimi kwenda kuomba msamaha Mtu Chee ni suala ambalo halimake sense,” Young Dee amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Mtu Chee mimi pamoja na uongozi wangu sijashauriwa kabisa na sidhani kama kuna siku kutakuwa na hili kundi. Mimi niwatakie kila lakheri katika safari yao ya kimuziki na nawaombea mafanikio huko mbeleni lakini mimi suala la kurudi sidhani kama lipo tena,” amesisitiza.

Wiki iliyopita Stamina alisema: Anytime kama ataona yeye ndio alikosea kama alivyorekebisha mistakes zake katika management yake, kama ataweza kurekebisha mistakes zake pia kwenye kundi anakaribishwa anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo tu ya kikazi na kipindi cha kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude yake hayo kwahiyo ndio maana ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na kusolve chochote,” aliongeza.

SOURCE: BONGO5

Friday, July 1, 2016

STAMINA ASEMA YOUNG DEE ANAWEZA KURUDI MTU CHEE

13531968_1101664066571243_1094846367_nKwa mujibu wa Stamina kuondoka kwa Young Dee kwenye kundi la Mtu Chee kulitokana na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.

Hivi karibuni Young Dee alithibitisha tetesi za kutumia madawa ya kulevya na kutangaza kuwa ameacha. Wiki hii ameachia ngoma yake mpya ‘Hands Up.’

“Kulikuwa na misunderstanding baina yake yeye na Country Boy,” Stamina alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.

“Anytime kama ataona yeye ndio alikosea kama alivyorekebisha mistakes zake katika management yake, kama ataweza kurekebisha mistakes zake pia kwenye kundi anakaribishwa anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo tu ya kikazi na kipindi cha kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude yake hayo kwahiyo ndio maana ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na kusolve chochote,” aliongeza.

“Lakini sasa hivi kama yupo competent kabisa anaona anaweza kusolve chochote anakaribishwa muda wote.”

Miezi kadhaa iliyopita Mtu Chee waliachia ngoma bila Young Dee na kumshirikisha Young Killer.

Monday, May 30, 2016

HUU NDIO UFAFANUZI WA MENEJA WA ALI KIBA KUHUSU 'ALI KIBA TV'

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi na msanii Ali Kiba, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’
kiba11
Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.

“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.

“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.

Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.

Source: Bongo5

Thursday, May 26, 2016

SNURA ANUSURIKA KICHAPO KISA CHURA

STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Chura’ juzikati akiwa kwenye shoo iliyofanyika Masasi, Mtwara alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutaka kupigwa na mashabiki kisa kikiwa eti ni kutokuimba Wimbo wa Chura ambao umefungiwa.
SNURA341
SNURA341
Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo lilijiri mida ya usiku katika ukumbi mmoja maarufu uliopo Masasi ambapo Snura alikuwa akifanya shoo hapo na alipotaka kumaliza, mashabiki walimtaka amalize na Wimbo wa Chura ndipo kizaazaa kilipoanzia na kutaka kumpiga.
Baada ya kunyaka ubuyu huo, Over Ze Weekend lilimnyanyulia simu Snura ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini alipopigiwa meneja wake, Hemed Kavu ‘HK’ alipokea na kukiri kutokea kwa tukio hilo.
“Siyo tukio moja tu, tulishaenda shoo zaidi ya mbili tunakutana na dhahama hizi. Tatizo lililopo, Snura hawezi kupafomu wimbo ule kwa kuwa ulizuiliwa kutokana na video yake. Ni muda umepita video mpya imetengenezwa na kupelekwa bodi ya filamu kukaguliwa lakini hawajatoa jibu lolote zaidi ya kuzungushwa tu, mara TCRA mara Basata,” alisema HK.
Chanzo: GPL

Friday, May 13, 2016

TIGO YAPINGA KUWALIPA AY, MWANAFA SH 2 BILIONI

Kampuni ya simu ya MIC Tanzania (Tigo) imekata rufaa kupinga hukumu iliyoamuru iwalipe Sh2 bilioni wanamuziki wawili, Ambwene Yesaya na Hamisi Mwinjuma kutokana na kutumia bila ya ridhaa yao, nyimbo za wasanii hao nyota nchini.

Yesaya, ambaye ni maarufu kwa jina la kisanii la AY na Mwinjuma anayejulikana kwa jina la MwanaFA, walifungua kesi hiyo ya madai kwenye Mahakama ya Wilaya ya Ilala kupinga kitendo cha kampuni hiyo ya huduma za simu kutumia nyimbo zao kwenye miito ya simu bila ya ridhaa yao.

Nyimbo mbili zilizotumika kwenye miito hiyo ya simu ni “Dakika Moja” na “Usije Mjini” ambazo nyota hao wameshirikiana.

Tuesday, May 10, 2016

AY na Mwana Fa kuishitaki kampuni inayotumia nyimbo zao bila ridhaa?

13129514_281332635540971_1875733816_nKuna uwezekano mkubwa, AY na Mwana FA wamefungua kesi ya masuala ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi zao.

Mwanasheria maarufu nchini, Alberto Msando amepost picha Instagram akiwa kwenye mahakamu kuu ya Tanzania akiwa na rappers hao. “At the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo #CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” ameandika Msando.

Kuna uwezekano kuwa nyimbo zao Usije Mjini na Dakika Moja zikawa zimetumiwa na kampuni hiyo bila ridhaa yao. Makosa ya kukiuka haki miliki kwenye kazi za sanaa huadhibiwa zaidi kwa kwa faini.
SOURCE: Bongo5

Ben Pol aipa albamu yake jina la mtoto wake

Ben Pol akiongea kwenye The Playlist
Msanii wa muziki wa R&B, Benard Paul ‘Ben Pol’, yupo katika maandalizi ya mwisho ya kuachia albamu yake aliyoipachika jina la mwanaye wa kwanza, ‘Mali’ aliyezaliwa hivi karibuni.

Akizungumza na gazeti la Mtanzania, Ben Pol amesema albamu hiyo itatoka katikati ya mwezi wa sita.

“Nimefanikiwa kukamilisha albamu yangu bila msaada wa mtu mwingine yeyote ndiyo maana nimeamua kuiita jina la mwanangu, ‘Mali’. Kwa sababu kila kitu nimefanya mwenyewe na kuenzi jina la mwanangu,” alisema Ben Pol.

Pia Ben Pol alisema kabla ya kuachia albamu hiyo anatarajia kuachia video ya wimbo ‘Moyo’ akiwa ameifanyia nchini Afrika Kusini chini ya mtayarishaji, Lolpop katika studio ya Tetemesha.

Monday, December 28, 2015

BEN POL AFICHUA SABABU YA AVRIL KUTOONEKANA KWENYE VIDEO YA NINGEFANYAJE


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijhKYS7OGNUPvggG7VrLO6XOQtjwTeJDjT0dA4YMYNdKcpS__6gLh728p8b3_QkWsunWGS3yw5BN2yeD81L6n2E0oLZFKfDw4mzDr7xWJhT0UhO1-itF4VTxhfH3sTUCkdr6oHmEmEniRX/s1600/48JwVIyK.jpeg
Siku chache baada ya kuachia video ya wimbo wake - ‘NINGEFANYAJE’, muimbaji wa R&B kutoka Tanzania, Bernard Paul  maarufu kama Ben Pol ameeleza sababu zilizopelekea muimbaji  Avril kutoka Kenya aliyeshirikishwa kwenye wimbo huo,  kutoonekana kwenye video hiyo anayoitaja kuwa kubwa kuliko video zote alizowahi kufanya.

Katika video hiyo iliyoongozwa na Justin Campos wa Afrika Kusini, Ben Pol anaonekana akiimba na Rossie M  ambaye pia ameshirikishwa kwenye wimbo huo huku mashabiki wakiisikia sauti ya Avril bila kumuona mwimbaji huyo mrembo.

Ben Pol amewaomba radhi mashabiki wake kwa kuwapa video ambayo haijakamilisha wahusika wote hususan kutokuonekana kwa Avril,  na kwamba sababu zilizopelekea hivyo zilikuwa nje ya uwezo wa pande zote katika utayarishaji wa video hiyo.

​​​Ben amesema kuwa baada ya yeye na Rossie M kuwasili Afrika Kusini ilikoshutiwa video hiyo, zilijitokeza changamoto muda mfupi kabla ya kuanza zoezi hilo. Ben Pol ameeleza kuwa pamoja na kuwa na maandalizi makubwa, video ya ‘Ningefanyaje’ ilikumbwa na changamoto nyingi tangu awali zilizopelekea kuahirishwa mara tatu.

“Kwa kweli hii video tokea mwanzo ilikuwa na changamoto, kwanza tuliisogeza mbele karibu mara tatu tena tukiwa tayari tumeshafika Afrika Kusini mimi na Rossie,” alisema Ben Pol. “Mara ya kwanza ni kutokana na ‘delay’ ya viza upande wa Avril. Si unajua Wakenya wao wanaenda South kwa viza tofauti na sisi Tanzania hatuendi kwa viza so kwetu ni rahisi zaidi muda wowote tu ukiamua fasta unaenda,” aliongeza.

Mkali huyo alieleza kuwa baada ya terehe mpya kupangwa na muongozaji aliyeshuti video hiyo, Justin Campos, siku moja kabla ya kushuti, AVRIL alipata tatizo lingine ambalo lilimzuia kusafiri kwa siku iliyofata kwenda Afrika Kusini.


Wakati huo huo, Campos naye alimueleza Ben Pol kuwa  kwa jinsi ratiba yake ilivyo endapo ataahirisha tena kushuti video hiyo, ratiba yake isingemruhusu kushuti video hiyo hadi Januari au Februari 2016,  kitu ambacho Ben Pol amesema  kisingewezekana kwasababu ingeendelea kumgharimu zaidi kifedha na kuvuruga ‘timing’ yake.

“Kutokana na hali hiyo, sikuwa na jinsi nyingine zaidi ya kukubali matokeo kwasababu  mwisho wa siku si mimi wala Avril wala director aliyekwamisha bali ni ‘situation’ ambayo ilikuwa nje ya uwezo wa kibinadamu.” Ben Pol anaeleza.

Ameongezea kuwa pamoja na kwamba angeweza kuamua kushuti video kwa kutumia version nyingine ya wimbo huo isiyokuwa na sauti ya Avril ili video isionekane na upungufu wake, lakini hakupenda kufanya hivyo kwa kuwa lengo kuu la wimbo lilikuwa kumshirikisha mwimbaji huyo. Pia, mashabiki wangekosa ladha nzuri na kazi nzuri aliyoifanya Avril.  Hivyo, aliamua kufanya video hiyo bila Avril na kukusudia kuwaeleza mashabiki wake kilichosababisha hali hiyo kwa kuwa aliamini mashabiki wataelewa magumu aliyopitia katika kuwapa video hiyo waliyokuwa wakiisubiri.

“Namshukuru sana Avril kwa kukubali kufanya kazi na mimi kwasababu imetimiza moja kati ya malengo yangu ya 2015, ambayo ilikuwa kuanza kufanya kazi na wasanii wa nje ya Tanzania na yeye ndiye alikuwa chaguo langu la kwanza. Ni imani yangu tutafanya tena project nyingine ya pamoja na kuikamilisha kama tulivyoikusudia,” alimaliza Ben Pol na kuwashukuru  mashabiki wake kwa kuupokea kwa mtazamo chanya wimbo na video yake.

ITAZAME VIDEO HAPA CHINI


Monday, December 30, 2013

Salamu za Mwisho wa Mwaka kutoka kwa msanii Dayna Nyange

Habari zenu ndugu. Kwanza napenda kumshukuru mwenyezi mungu anayetupa pumzi bila malipo, kwani yeye ndiyo kila kitu. Naishkuru familia yangu kwa kunipa moyo kila kukicha mpaka hapa leo hii. Napenda kutoa shukrani kwenu ndugu zangu kwa kunisapot katika kazi zangu na ushauli wa kila leo. 

Tunakutana na mitihani mingi sana lakini mungu anawapa moyo wa kuwa nami pamoja. shukrani sana kwa vyombo mbalimbali vya habari kwa mwaka mzima kuendelea kunisapot kwa kila hali. 

Radio na Tv mbalimbali kwa kutenga muda wa kupiga nyimbo zangu na kunipa interview juu ya kazi zangu. nawashkuru sana . Studio mbalimbali kwa kuweza kunipa nafasi ya kufanya kazi katika studio izo. 

Pia Bloggs na website  na Magazeti mbalimbali, mmtenga muda wenu kwa kuthamini kazi za Dayna Nyange mmeonesha ushirikiano mkubwa sana kwangu. niwashukuru waandaaji wa matamasha  kwa kunipa nafasi ya kufanya show katika matamasha hayo, ni jinsi gani mnavyoonesha kujali kazi zangu na kunipa moyo. 

Lakini pia watangazaji na ma dj wa Radio husika mmekuwa mkitenga muda wa kuwa  nami katika kazi zenu,Niwashkuru sana Ma requester wote Tanzania na nje ya Tanzania kwa ku request nyimbo zangu na kupata nafasi ya kupigwa katika media izo. Nyinyi ni mchango mkubwa sana kwa sanaa yetu .Mafans wangu mnaozidi moyo na kunishauli juu ya kazi zangu na maisha kwa jumla kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano. 

Tunafunga mwaka 2013 na tunaamia mwaka 2014  Sitawaangusha.. Mwaka 2013 , tumepoteza ndugu zetu tuliokuwa nao ktk tasnia hii. Tuzidi kumuomba mungu azipumzishe roho zao mahali pema Albert mangwea, Langa kileo, marc malim Sharomilionea, Sajuki,na wengine wote wapumzike kwa amani. 

Nichukue nafasi hii kuomba radhi kwa wote niliowakosea au kukoseana kwani ni madhaifu ya kibinaadam. Lakini pia niseme tu kwa wote walionikosea Nimewasamehe bila kinyongo chochote na kwa dhati toka moyoni mwangu. Tusahau yaliyopita tuanze mwaka tukiwa Safi. Tumuombe mungu atupe afya njema na mafanikio zaidi  mwaka 2014 na Kuendelea. Amina.