
Rapper Rick Ross na bosi wa Maybach Music Group, amemsaini rapper
asiyekuwa na makazi aliyekutana naye barabarani na kuanza kuchana mbele
yake ili kupata nafasi ya kuwa kwenye lebo yake.
Isa Muhammad ni rapper asiyekuwa na makazi ya kuishi na kwao ni
California ambaye amekuwa na bahati ya mtende kwa kulifurahisha sikio la
Rozay na kuwa msanii mpya wa MMG.
Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, Rozay amesema hakutegemea
kumsaini msanii huyo ila uwezo na moyo wake ulimfanya iwe rahisi
kumkubali.

0 comments:
Post a Comment