
Hapo awali Mubenga alisema aliamua kuachana na Ommy Dimpoz ili na
yeye afanye mambo yake bifansi pamoja na kuanzisha label yake mpya ya
muziki itayokuwa inasimamia wasanii.
“Kiukweli ni kwamba hakuna tatizo, ni mambo ya kazi PKP ni kama
nyumbani tu, nimeamua kuhama nyumbani na kwenda kuanzisha maisha yangu,”
Mubenga alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Hakuna kudhurumiana, hiyo
stori ndo naisikia kwako, hakuna kitu kama hicho, na mimi sina tatizo
na Ommy Dimpoz,”
Mubenga kwa sasa ameanzisha label yake mpya ‘Bengaz Entertainment’ ambayo itaanza kusaini wasanii wa muziki hivi karibuni.
Source: Bongo5.com
0 comments:
Post a Comment