Thursday, August 4, 2016

MSANII UDE UDE AFARIKI DUNIA TANGA


Msanii na mtunzi wa nyimbo za Bongo Fleva,Hamid Hafidhi maarufu kama Ude Ude na rafiki yake Iku wamefariki dunia wakiwa mkoani Tanga.
Marehemu Ude Ude na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo enzi za uhai wao
Marehemu Ude Ude na rafiki yake Iqu Junior ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo enzi za uhai wao
Marehemu Ude Ude alijipatia umaarufu kwenye muziki wa bongo fleva kwa umahiri wake wa kuwatungia nyimbo wasanii ambapo nyimbo alizozitunga ni pamoja naWangu na Yahaya za Lady Jay dee,Ballin and Chillin ya Sammisago.
Ude Ude na Iqu Junior wanadaiwa kuuawa katika tukio la ujambazi lilitokea mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wawili hao walikuwa miongoni mwa majambazi wanne waliokuwa na gari aina ya Toyota Probox waliokurupushwa na polisi katika jaribio la kuiba vifaa vya magari ya halmashauri.

Tukio hilo lilitokea jana saa mbili asubuhi walipokutwa wakivunja gari la mwalimu wa shule ya sekondari, Maweni aliyejulikana kwa jina la Dominica Tarimo.

Wananchi wakiwa na piki piki na magari pia waliungana na polisi kuwafukuza watu hao na kuwashambulia. 
Polisi hao wamedai watu hao walijihami na silaha zenye ncha kali ili kujiokoa na wawili kupiga risasi huku wawili wakitokomea kwenye msitu ulio jirani na kiwanda cha saruji cha Sungura.
Hapa chini nimekuwekea taarifa hiyo ya gazeti la Mwananchi.
10d2cf02-3ce6-489c-ae4a-e05f0114530d.jpg
R.I.P Rafiki Zetu, Roho za Marehemu zilale mahali pema peponi Amen.

0 comments:

Post a Comment