
Habari
zenu ndugu. Kwanza napenda kumshukuru mwenyezi mungu anayetupa pumzi
bila malipo, kwani yeye ndiyo kila kitu. Naishkuru familia yangu kwa
kunipa moyo kila kukicha mpaka hapa leo hii. Napenda kutoa shukrani
kwenu ndugu zangu kwa kunisapot katika kazi zangu na ushauli wa kila
leo.
Tunakutana
na mitihani mingi sana lakini mungu anawapa moyo wa kuwa nami pamoja.
shukrani sana kwa vyombo mbalimbali vya habari kwa mwaka mzima kuendelea
kunisapot kwa kila hali.
Radio
na Tv mbalimbali kwa kutenga muda wa kupiga nyimbo zangu na kunipa
interview juu ya kazi zangu. nawashkuru sana . Studio mbalimbali kwa
kuweza kunipa nafasi ya kufanya kazi katika studio izo.
Pia
Bloggs na website na Magazeti mbalimbali, mmtenga muda wenu kwa
kuthamini kazi za Dayna Nyange mmeonesha ushirikiano mkubwa sana
kwangu. niwashukuru waandaaji wa matamasha kwa kunipa nafasi ya kufanya
show katika matamasha hayo, ni jinsi gani mnavyoonesha kujali kazi
zangu na kunipa moyo.
Lakini
pia watangazaji na ma dj wa Radio husika mmekuwa mkitenga muda wa kuwa
nami katika kazi zenu,Niwashkuru sana Ma requester wote Tanzania na nje
ya Tanzania kwa ku request nyimbo zangu na kupata nafasi ya kupigwa
katika media izo. Nyinyi ni mchango mkubwa sana kwa sanaa yetu .Mafans
wangu mnaozidi moyo na kunishauli juu ya kazi zangu na maisha kwa jumla
kupitia vyanzo vyangu vya mawasiliano.
Tunafunga
mwaka 2013 na tunaamia mwaka 2014 Sitawaangusha.. Mwaka 2013 ,
tumepoteza ndugu zetu tuliokuwa nao ktk tasnia hii. Tuzidi kumuomba
mungu azipumzishe roho zao mahali pema Albert mangwea, Langa kileo, marc
malim Sharomilionea, Sajuki,na wengine wote wapumzike kwa amani.








0 comments:
Post a Comment