Rapper Young Dee amesema suala la yeye kuwapigia magoti Stamina na
Country Boy ili arudi kwenye kundi la Mtu Chee ‘halimake sense.’
Stamina alidai kuwa kutoka kwa Young Dee kwenye kundi hilo kulitokana
na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama
atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.
“Suala la mimi kwenda kuomba msamaha Mtu Chee ni suala ambalo halimake sense,” Young Dee amemuambia mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Mtu Chee mimi pamoja na uongozi wangu sijashauriwa kabisa na sidhani
kama kuna siku kutakuwa na hili kundi. Mimi niwatakie kila lakheri
katika safari yao ya kimuziki na nawaombea mafanikio huko mbeleni lakini
mimi suala la kurudi sidhani kama lipo tena,” amesisitiza.
Wiki iliyopita Stamina alisema: Anytime kama ataona yeye ndio
alikosea kama alivyorekebisha mistakes zake katika management yake, kama
ataweza kurekebisha mistakes zake pia kwenye kundi anakaribishwa
anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo tu ya kikazi na kipindi cha
kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude yake hayo kwahiyo ndio maana
ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na kusolve chochote,” aliongeza.
SOURCE: BONGO5
Monday, July 4, 2016
HIKI NDICHO YOUNG DEE ALICHOWAJIBU MTU CHEE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment