Kwa mujibu wa Stamina kuondoka kwa Young Dee kwenye kundi la Mtu Chee
kulitokana na kupishana kauli kati yake na Country Boy, na kwamba kama
atarekebisha makosa aliyowafanyia wako radhi kumrejesha kundini.
Hivi karibuni Young Dee alithibitisha tetesi za kutumia madawa ya
kulevya na kutangaza kuwa ameacha. Wiki hii ameachia ngoma yake mpya
‘Hands Up.’
“Kulikuwa na misunderstanding baina yake yeye na Country Boy,” Stamina alimweleza mtangazaji wa Jembe FM, JJ.
“Anytime kama ataona yeye ndio alikosea kama alivyorekebisha mistakes
zake katika management yake, kama ataweza kurekebisha mistakes zake pia
kwenye kundi anakaribishwa anytime hakuna mtu mwenye bifu naye ni mambo
tu ya kikazi na kipindi cha kati alipokuwa amechanganyikiwa na madude
yake hayo kwahiyo ndio maana ilikuwa ni ngumu kuweka kukaa chini na
kusolve chochote,” aliongeza.
“Lakini sasa hivi kama yupo competent kabisa anaona anaweza kusolve chochote anakaribishwa muda wote.”
Miezi kadhaa iliyopita Mtu Chee waliachia ngoma bila Young Dee na kumshirikisha Young Killer.
Friday, July 1, 2016
STAMINA ASEMA YOUNG DEE ANAWEZA KURUDI MTU CHEE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment