![]() |
Baadhi ya Mashabiki wakiwa Airport kuupokea mwili wa marehemu Ngwair |
![]() |
Professor Jay akifanya Interview, kulia ni Producer Lamar |
![]() |
Hapa ni safari ya kuelekea ilipoanza |
![]() | |||||
Lamar na Jay Moe |
IKIWA ni leo ndiyo mwili wa Marehemu wa Albert Mangwea umewasili nchini, maelfu ya mashabiki wamejitokeza kuupokea mwili wa msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya.
Katika mapokezi hayo watu walikuwa wengi zaidi kiasi cha mashabiki wake hao kupingana na kauli ya polisi waliotaka gari lililobeba mwili wa marehemu Ngwair kuendeshwa lakini wao walitaka kulisukumu gari hilo mpaka hospitali ya Taifa Muhimbili na wengine wakitaka jeneza litolewe ili walibebe kwa mikono mpaka Muhimbili.
Mashabiki hao waliojipanga pembezoni mwa barabara kushuhudia mwili wa mpendwa wao Ngwair, licha ya wengi wao kushuhudia gari lililobeba jeneza lenye mwili wa Ngwair lakini miongoni mwao walionekana bado hawaamini kama kweli msanii huyo amefariki.
Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi, Aminnnnn!!!
0 comments:
Post a Comment