Showing posts with label Paul Walker. Show all posts
Showing posts with label Paul Walker. Show all posts

Tuesday, December 10, 2013

Maziko ya Paul Walker kuhudhuriwa na wanafamilia tu

Mazishi ya  Paul Walker yanatarijiwa kuwa ya binafsi ... ambapo imeelezwa itakuwa ni kwa ajili ya familia tu, pamoja na baadhi ya crew ya fast & Farious.

Vyanzo vya karibu vyenye uhusinano na familia ya Walker viliiambia TMZ kuwa wasiwasi wao mkubwa ni binti wa Walker mwenye umri wa miaka 15  Meadow, ambaye kwa kwa sasa yupo katika wakati mgumu, hivyo familia hiyo hawataki kundi kubwa la watu kuwa jirani na binti huyo, kwa sababu anahitaji kujisikia vizuri na kuondokana na huzuni aliyonayo.
Hivyo mazishi ya Walker yatakuwa na mwaliko maalumu kwa watu watakaopewa, na pia inaelezwa kuwa baada ya mazishi kutakuwa na kumbukumbu itakayofanyika lakini pia itakuwa ni kwa mwaliko.

Saturday, December 7, 2013

Paul Walker, gari ya ndoto yake ndiyo imemuua

Miaka minne kabla ya kifo chake, Paul Walker alizungumza katika interview na kesuma kuwa gari ya ndoto yake ni Porsche Carrera GT ...gari ambayo amekufa akiwa ndani yake.

Paul aliyasema maneno hayo wakati akifanya interview ya kuitangaza Fast &Farious mwaka 2009, ambapo alisema gari hiyo iko mawazoni mwake.
Paul amekufa akiwa ndani ya gari hiyo wiki iliyopita, yeye pamoja na dereva aliyekuwa akiendesha gari hiyo, ambapo iligonganga mti.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI



Monday, December 2, 2013

Universal Pictures, wadai kifo cha Paul Walker ni pigo kubwa kwao



Kampuni ya utengezaji filamu ya 'Universal Pictures', ambao ndiyo wazalishaji wa mfululizo wa filamu za Fast & Farious imetoa neno baada ya kifo cha mwigizaji Paul Walker.

Sehemu ya taarifa uiliyotolewa na kampuni hiyo inasema, "Wote sisi ndani ya Universal tumepata mshituko mkubwa sana".

"Paul alikuwa ni mmoja ya watu ambao alikuwa anapendwa na kuheshimiwa ndani ya familia ya studio yetu kwa muda wa miaka 14, pigo hili si kwetu pekee bali kwa kila mtu ambaye ameshiriki filamu ya Fast & Farious, na mashabiki wote," alieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Universal iliongeza, "Tunatuma salama za rambirambi kwa dhati kabisa kwa familia ya Paul,".

Walker (40) ameacha binti wa miaka 15.

Huyu ndie star wa fast & Farious aliyekufa kwa ajali



Mwigizaji Paul Walker alikufa katika ajali ya gari siku ya Jumamosi huko Kaskazini mwa Los Angeles, Marekani.

Star huyo wa fast and Farious alikuwa ni abiria katika gari aina ya Porsche, ambapo gari hilo linasadikiwa kugonga mti au ukingo, na kupasuka na moto kuwaka. imethibishwa hivyo.

Walker (40) pamoja na mtu mwingine walikufa katika eneo la tukio

"Kwa moyo wa majonzi lakini ni lazima kuthibitisha kwamba Paul Walker amefariki leo katika ajali ya gari, aliyoipata wakati akienda kuhudhuria Charity event kwa ajili ya shirika lake la Reach Out Worldwide. Yeye alikuwa ni abiria katika gari ya rafiki yake, ambapo wote walipoteza maisha yao".

"Tunashukuru na tunatakiwa kuwa wavumilivu kwa habari hii ambayo imetusikitisha. Tuwe pamoja na familia na marafiki katika maombi yao katika wakati huu mgumu, "alisema mwakilishi ambaye hata hivyo hakutajwa jina lake.