Monday, December 2, 2013

Huyu ndie star wa fast & Farious aliyekufa kwa ajali



Mwigizaji Paul Walker alikufa katika ajali ya gari siku ya Jumamosi huko Kaskazini mwa Los Angeles, Marekani.

Star huyo wa fast and Farious alikuwa ni abiria katika gari aina ya Porsche, ambapo gari hilo linasadikiwa kugonga mti au ukingo, na kupasuka na moto kuwaka. imethibishwa hivyo.

Walker (40) pamoja na mtu mwingine walikufa katika eneo la tukio

"Kwa moyo wa majonzi lakini ni lazima kuthibitisha kwamba Paul Walker amefariki leo katika ajali ya gari, aliyoipata wakati akienda kuhudhuria Charity event kwa ajili ya shirika lake la Reach Out Worldwide. Yeye alikuwa ni abiria katika gari ya rafiki yake, ambapo wote walipoteza maisha yao".

"Tunashukuru na tunatakiwa kuwa wavumilivu kwa habari hii ambayo imetusikitisha. Tuwe pamoja na familia na marafiki katika maombi yao katika wakati huu mgumu, "alisema mwakilishi ambaye hata hivyo hakutajwa jina lake.

0 comments:

Post a Comment