Kampuni ya utengezaji filamu ya 'Universal
Pictures', ambao ndiyo wazalishaji wa mfululizo wa
filamu za Fast & Farious imetoa neno baada ya kifo cha mwigizaji Paul
Walker.
Sehemu ya taarifa uiliyotolewa na kampuni hiyo inasema, "Wote sisi ndani ya Universal
tumepata mshituko mkubwa sana".
"Paul alikuwa ni mmoja ya watu
ambao alikuwa anapendwa na kuheshimiwa ndani ya familia ya studio yetu kwa muda
wa miaka 14, pigo hili si kwetu pekee bali kwa kila mtu ambaye ameshiriki
filamu ya Fast & Farious, na mashabiki wote," alieleza sehemu ya
taarifa hiyo.
Taarifa hiyo ya Universal iliongeza, "Tunatuma salama za rambirambi kwa dhati kabisa kwa familia ya
Paul,".
Walker (40) ameacha binti wa miaka 15.
0 comments:
Post a Comment