Showing posts with label Jakaya Kikwete. Show all posts
Showing posts with label Jakaya Kikwete. Show all posts

Saturday, March 22, 2014

Rais Kikwete alipohutubia Bunge, Soma na Hotuba yake hapa

 Rais Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum
 Rais Kikwete akisisitiza jambo katika hotuba yake
Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda akifurahia jambo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Pandu Ameir Kificho, na Mhe Mohamed Seif Khatib na wajumbe wengine. PICHA NA IKULU

=======  =======  =======
SOMA HAPA CHINI HOTUBA YAKE


  
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma leo
 Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassa Mwinyi na wajumbe wakifuatilia hotuba ya Rais Kikwete leo
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Makungu na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe Amani Abeid Karume na wajumbe wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete leo 
 Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe Tundu Lissu akigonga meza kuashiria kukunwa na hotuba ya Rais Kikwete
 Mjumbe wa Bunge Maalum Mhe Freeman Mbowe akishangilia hotunba ya Rais Kikwete.

Monday, December 16, 2013

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA SIDO

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Eng. Omari Jumanne Bakari kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogovidogo (SIDO).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo umeanza Desemba 04, mwaka huu, 2013. Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtafiti Mwandamizi katika Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam.

Eng. Omari Jumanne Bakari ni Mtanzania mwenye elimu, weledi na uzoefu ambao umemfanya Mheshimiwa Rais aamini kuwa atakapoongoza SIDO, atasaidia kukidhi matarajio ya taifa kwa kueneza ujasiriamali, uwekezaji,uzalishaji na kutoa nafasi za ajira katika ngazi ya viwanda vidogo na vya kati kama msingi imara wa uchumi wa Tanzania, ikiwemo kwa kuingiza sayansi, teknolojia na ubunifu katika viwanda vidogo vidogo.
         “Mwisho”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR ES SALAAM.

16 Desemba, 2013

HOTUBA YA RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA MZISHI YA MANDELA

Monday, December 9, 2013

Soma hapa jinsi Nelson Mandela alivyosahau viatu vyake alipokuja Tanzania

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewataka watanzania kuacha tabia ya kuwa na roho ya kulipiza visasi badala yake wawe watu wa kusamehe na kusahau kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanamuenzi moja kwa moja Rais mstaafu wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela.
Rais Kikwete amesema mara baada ya Rais Mandela kutolewa gerezani  hofu ilitawala Afrika ya Kusini, watu wengi wakitambua kuwa atakapochaguliwa kuwa Rais badala ya kuijenga nchi ataanza kulipiza visasi kwa wale wote waliotumika kwa namna moja ama nyingine kumtesa yeye na watu wa nchi yake.
“Badala yake Mzee Mandela alitoa tamko la kuwasamehe wote waliohusika kuwabagua watu wa Afrika ya Kusini, na kisha aliunda tume maalumu ya maridhiano ili kujenga umoja kati ya watu wenye ngozi nyeupe na wenye ngozi nyeusi, jambo hili ni la ajabu sana” amesema Kikwete.
“Hiki ni kipimo kikubwa cha ukomavu wa kisiasa, yatupasa watanzania na viongozi mbalimbali kuenzi jambo hili la kusameheana na kutokuwa walipiza visasi, hapa tulipo wengine wanasema kabisa nikichaguliwa watanikoma….. lakini nawasihi tumuenzi Mzee Mandela kwa kuiga mambo mema aliyoyafanya ambayo hadi hivi leo yamechangia kukuza uchumi wa Afrika ya Kusini, “amesema Kikwete.
Amesema tokea enzi za TANU Tanzania imekuwa karibu sana na vyama vya ukombozi wa mataifa mengi Afrika, kikiwemo chama cha ANC ambacho kilikuwa kikiongozwa na Marehemu Mzee Mandela, hivyo aliwasihi watanzania waendeleze umoja huo .
“Kuna jambo moja ambalo hamlijui mwaka wa 1964 Mzee Mandela alikuja nchini na kufikia kwa mweka hazina wa TANU, Siro Swai, alikuwa akielekea kwenye mafunzo ya kijeshi Algeria, aliacha viatu vyake ‘pea moja’ akieleza kuwa atakaporudi atakuja kuvichukua lakini haikuwa hivyo, nilipokuwa waziri wa mambo ya nje, mke wa Swai alinifuata na kunieleza, nasi tulilazimika kuzirudisha kipindi hicho ambacho Mzee Mandela alikuwa Rais wa nchi hiyo tayari,” Anaeleza Kikwete.
Amesema haya yote yanatafsiri ukaribu na undugu wa hali ya juu kati ya nchi zetu mbili na ndiyo maana katika kumuenzi leo hii kwenye shughuli za kutimiza miaka 52 ya uhuru hatutakuwa na vikundi vya kutumbuiza.

Friday, December 6, 2013

Rais Kikwete Atuma Salamu za Rambirambi kifo cha Mandela

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425

PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za rambirambi Rais Jacob Zuma wa Afrika ya Kusini  na kupitia kwake, kwa mkewe Bi. Graca Machel, wanafamilia wote na wananchi wote wa Afrika ya Kusini kufuatia kifo cha Mzee Nelson Mandela kilichotokea  tarehe 5 Desemba, 2013 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Rais ameuelezea msiba huu kuwa ni msiba mkubwa kwetu sote.
"Afrika ya Kusini, Afrika na dunia kwa ujumla imepoteza mtu mashuhuri na shujaa mkubwa wa Karne ya 20 na 21.Tunaelewa  machungu waliyonayo wananchi wa Afrika ya Kusini kwa kupoteza kiongozi shupavu, jasiri, mwana mapinduzi , mvumilivu na mstahimilivu".
Ameongeza Rais Kikwete.

Rais amemuelezea  Mzee Mandela kuwa ni  kielelezo cha aina yake kwa wanadamu kwa moyo wake wa kusamehe, huruma na upendo uliomuwezesha  kuwaunganisha wananchi wa Afrika ya Kusini kuwa  taifa moja baada ya kipindi kirefu cha mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

"Mandela  ni mfano bora kwa wanadamu wa  jinsi binadamu muungwana anavyopaswa kuwa . Ni wajibu wa wana Afrika Kusini, Afrika na dunia kwa jumla kuiga mfano wake hasa moyo wake wa uzalendo, kujitolea hata maisha yake kwa ajili yake na wananchi wenzake" .Rais ameongeza kusema, "Tuzidi kumuombea kwa Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mzee Mandela  mahali pema peponi".


Kufuatia kifo hicho Rais ametangaza siku 3 za maombolezo kuanzia leo tarehe 6 hadi 8 Disemba, 2013.

Aidha, Mheshimiwa Rais ameagiza  kuwa katika siku hizo 3 bendera zote zipepee  nusu mlingoti.

Mwisho.
Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu,
DAR AS SALAAM.
06 Desemba,2013

Friday, November 29, 2013

Hivi ndivyo Rai Kikwete alivyopokea Kombe la Dunia

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilifunua na kulinyanyua Kombe la Dunia katika uwanja wa michezo Kirumba mjini Mwanza leo jioni. Kombe hilo limerejea jijini Dar es Salaam na kesho wananchi watapata fursa ya kupiganalo picha.

Tuesday, November 5, 2013

RAIS KIKWETE AKIKARIBISHWA NA RAIS JACOB ZUMA KATIKA MKUTANO WA PAMOJA WA SADC NA ICGLR

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa na Rais Jacob Zuma katika mkutano wa pamoja wa SADC NA ICGLR katika ukumbi wa kimataifa wa Oliver Tambo jijini Pretoria, Afrika Kusini, usiku wa kuamkia leo Oktoba 5, 2013.

Friday, October 18, 2013

RAIS KIKWETE AZINDUA KIWANDA CHA CHAI NJOMBE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, amezindua rasmi Kiwanda cha Kusindika Chai cha Ikanga, Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya  Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa asilimia 25 na wakulima wa chai wa Lupembe ni ukombozi mkubwa wa wakulima wa Tarafa ya Lupembe ambao wamekuwa wanakabiliwa na ukosefu wa sehemu ya kuuza chai yao.
Ufunguzi wa kiwanda hicho cha Ikanga Tea Factory kinachomilikiwa na Kampuni ya Ikanga Tea Factory Limited ni utekelezaji wa ahadi ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anafanya kampeni ya Urais katika Tarafa ya Lupembe mwaka 2010. Ni kiwanda kipya zaidi na bora zaidi cha kusindika chai katika Tanzania.
Ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mwishoni mwa mwaka 2010 baada ya Serikali ya Rais Kikwete Mei mwaka huo huo kuiomba Kampuni ya Mufindi Tea and Coffee Limited (MTC) kujenga kiwanda cha kusindika chai ya wakulima ambayo sehemu yake kubwa ilikuwa inapotea na kuoza kwa sababu ya ukosefu wa kiwanda.
Ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho, MTC iliunda kampuni mpya ya Ikanga Tea Company Limited Septemba 2010. Kampuni hiyo ni ubia kati ya MTC na wakulima wa chai wa Lupembe ambao wanamiliki asilimia 25 za hisa za kiwanda hicho kupitia umoja wao wa Lupembe Tea Farmers Trust.
Uzinduzi wa leo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda hicho. Chini ya awamu hiyo ya kwanza yenye uwezo wa kusindika tani 1,800 za chai kwa mwaka kwa kutumia njia moja ya uzalishaji iliyokamilika  Juni mwaka jana kwa gharama ya Sh. bilioni  3.75. Awamu ya pili ambayo inaendelea kujengwa, itagharimu Sh. bilioni 1.48 na ikikamilika kiwanda kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 3,500 na awamu ya tatu na ya mwisho itagharimu Sh.bilioni 1.5 na kukamilika kwa awamu hiyo kutakiwezesha kiwanda kusindika tani 5,000 za chai kwa mwaka.
Chini ya uendeshaji wa Kiwanda hicho, chai yote ya wakulima inanunuliwa kwenye vituo maalum na kusafirishwa kwenda kiwandani na magari ya Kiwanda. Wakulima pia wanapewa mbolea kwa mkopo na wakulima wote wa chai inayochukuliwa na kiwanda hulipwa kila mwezi kwa bei iliyopangwa na Bodi ya Chai Tanzania.
Miongoni mwa mipango ya Kampuni ya Chai ya Ikanga ni kununua angalau hekta 600 za ardhi ili nayo ianze kulima chai ili kuongeza kiwango cha chai kinachozalishwa katika eneo la Lupembe na ukamilishaji wa shule kwa ajili ya watoto wa wakulima wa eneo la Lupembe.
Rais Kikwete amezindua Kiwanda hicho ikiwa ni shughuli ya kwanza katika shughuli nyingi ambazo atazifanya wakati wa ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Njombe kuzindua na kukagua shughuli za maendeleo. Miongoni mwa shughuli hizo itakuwa ni kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2013

Monday, September 16, 2013

Rais Kikwete ziarani nchini Marekani na Canada

Monday, August 5, 2013

MSAJILI WA VYAMA ASTAAFU, RAIS KIKWETE AMTEUA JAJI MUTUNGI KUSHIKA NAFASI YAKE

Jaji Francis S.K.Mutungi.Picha kwa hisani ya Robert Okanda.
========   =========  =========
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
             press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Jaji Francis S.K.Mutungi kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa.

Taarifa iliyotolewa Dar Es Salaam leo, Jumatatu, Agosti 5, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa uteuzi huo ulianza Ijumaa iliyopita Agosti 2, 2013.

Jaji Mutungi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Mhe. John Tendwa ambaye amestaafu Utumishi wa Umma kwa mujibu wa sheria.

Kabla ya uteuzi huo, Jaji Mutungi alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.