NYOTA
wa Hip Hop nchini Joseph Haule maarufu
kama Professa Jay amesema ujumbe ulioko kwenye wimbo wa msanii wa Arusha Jacob
Makala maarufu kama JCB umemgusa, hivyo kuamua kushirikiana naye katika
kuelimisha jamii.
Akizungumza
na gazeti hili, Professa Jay alisema wimbo huo unaofahamika kama ‘Drive Slow”
unahamasisha madereva wote nchini kuendesha vyombo vya usafiri taratibu ili
kuokoa maisha ya watu wanaogongwa na kufa na wengine wakibaki na ulemavu wa
maisha.
“Madereva
wengi wamekuwa wakiendesha magari au pikipiki kwa kasi bila kuangalia watu
wengine wanaotembea kwa miguu, kiasi kwamba huwagonga na kusababisha vifo,
hivyo nimeamua kushirikiana na JCB
katika kuhamasisha jamii kubadilika ili kuokoa maelfu ya watu,”alisema.
Professa
Jay ambaye alimpoteza mama yake mzazi kwa ajali, alisema aliguswa na ujumbe huo
na anaamini wengi wakiusikia watajifunza na kubadilika mara moja.
Licha
ya wimbo huo kumgusa, alisema JCB ni msanii anayemkubali na amekuwa na ndoto ya
kufanya kazi pamoja kwa muda mrefu ndio maana wameamua kushirikiana kutimiza
malengo ya msanii huyo.
0 comments:
Post a Comment