Thursday, October 3, 2013

Young Killer Akerwa na Simu za Mademu

 
MSANII wa kizazi kipya Erick Msodoki maarufu kama ‘Young Killer’ amewaonya baadhi ya watu ambao humpigia simu na kumsumbua bila sababu za msingi, kuacha tabia kwa vile humkera.
Msodoki alisema anashangazwa na baadhi ya watu hasa wanawake wamekuwa wakimpigia simu, wengine wakimtaka kimapenzi kitendo ambacho hakimfurahishi na ni kero.
 “Siku hizi kuna baadhi ya wanawake wananipigia simu wakinitaka, naomba waache tabia hiyo, sipendi usumbufu, kwani mimi bado mdogo, naomba mniache,”alisema.
Msanii huyo ambaye kwa sasa anavuma na ‘Mrs Superstar’ alisema anashangazwa watu hao wamepata wapi namba yake, kwasababu hakuigawa hadharani kwa kukwepa usumbufu wa aina hiyo.
Alisema ni bora kama wangekuwa wanapiga simu kumuunga mkono kwenye kazi zake, kuliko kumpigia simu na kumweleza mambo ambayo hayaendani na umri wake.

0 comments:

Post a Comment