Showing posts with label Professor Jay. Show all posts
Showing posts with label Professor Jay. Show all posts

Monday, October 21, 2013

Mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay akabidhiwa Barcode yake leo

Mwanamuziki Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.

Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya Barcode. Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.

Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa wanamuziki wa Tanzania kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.

Aidha Mwenyekiti Mmari alitanabaisha kuwa wanamuziki wa Tanzania hawawezi kuingia kwenye chati kubwa kama za Billboard bila kuwa na utambulisho wa ki electroniki wa Alama za Mistari yaani Barcode. Naye Afisa muandamizi wa GS1 Tanzania Bw. Pius Mikongoti alisema kuwa ni vigumu kupata takwimu sahihi za usambazaji za wanamuziki wa Tanzania kwani kazi zao haziko kwenye mfumo rasmi, “ukiangalia mwanamuziki kama Lady Jay Dee mathalani ana wafuasi wamefikia laki moja kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook kama atatangaza kuuza kazi zake kwenye mitandao hiyo ni wazi atawafiukia washabiki wake kirahisi zaidi” Takwimu za Billboard zinachukuliwa kutokana na usambazaji na mauzo ya kazi za mwanamuziki ki electroniki, ni vigumu kwa mwanamuziki kama Diamond ambaye kwa sasa ana mashabiki lukuki na kazi zake kupigwa kila kona kupata takwimu sahihi za usambazaji wake.

Aidha amewataka wadau wa muziki nchini kuacha kusambaza nyimbo mpya za wanamuziki kwenye mitandao na kuwafanya watu waweze kuzipata bila kuzitolea chochote (downloads), kwa kufanya hivyo tunawaumiza wanamuziki na tunakuwa hatuwasaidiii aliongeza Bw. Mikongoti. GS1 Tanzania ndio watoaji pekee wa huduma za BArcode kwa bidhaa zote za Tanzania, ikumbukwe kuwa ili uweze kuuza kwenye Supermarket na masoko ya mitandaoni ni lazima uwe na alama hizi za mistari yaani Barcode. 
 Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti) akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka Profesa Jay.
 Mwenyekiti wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.

Thursday, October 3, 2013

Profesa Jay Ampigia Salute JCB


NYOTA wa Hip Hop  nchini Joseph Haule maarufu kama Professa Jay amesema ujumbe ulioko kwenye wimbo wa msanii wa Arusha Jacob Makala maarufu kama JCB umemgusa, hivyo kuamua kushirikiana naye katika kuelimisha jamii.
Akizungumza na gazeti hili, Professa Jay alisema wimbo huo unaofahamika kama ‘Drive Slow” unahamasisha madereva wote nchini kuendesha vyombo vya usafiri taratibu ili kuokoa maisha ya watu wanaogongwa na kufa na wengine wakibaki na ulemavu wa maisha.
“Madereva wengi wamekuwa wakiendesha magari au pikipiki kwa kasi bila kuangalia watu wengine wanaotembea kwa miguu, kiasi kwamba huwagonga na kusababisha vifo, hivyo nimeamua  kushirikiana na JCB katika kuhamasisha jamii kubadilika ili kuokoa maelfu ya watu,”alisema.
Professa Jay ambaye alimpoteza mama yake mzazi kwa ajali, alisema aliguswa na ujumbe huo na anaamini wengi wakiusikia watajifunza na kubadilika mara moja.
Licha ya wimbo huo kumgusa, alisema JCB ni msanii anayemkubali na amekuwa na ndoto ya kufanya kazi pamoja kwa muda mrefu ndio maana wameamua kushirikiana kutimiza malengo ya msanii huyo.

Thursday, March 7, 2013

NEW TRACK: Lady Jay Dee Ft Professor Jay - Joto, Hasira

Bofya hii link kusikiliza

Mtunzi/ Mwandishi: JUDITH WAMBURA - JideJayDee
Mtunzi/Mwandishi Rap: JOSEPH HAULE - Prof Jay
Producer:  MAN WATER 
Studio: COMBINATION SOUND
Executive Producer: GARDNER G HABASH

Chorus:
Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa

VERSE 1:
Kila siku nimenuna
Kwanini tunagombana
Tena tunakosoana, kama tumechanganyikiwa
Na sioni hata maana
Ya si kuzinguana
Yaani kila mtu anajua sana
Au yote sababu ya?, sababu ya?

Rudia Chorus:

VERSE 2:
Mazao twalima wote
Sahani wavuta kwako
Kama chakula tule wote
Kwanini chote kije kwako
Kisu mpini umeshika wewe
Vitisho kunikata mimi mmmmhh
Au yote sababu ya? Sababu ya?

Chorus:
Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa

Hook:
Uuuuh, sahau sahau shida
Oooh ishi ka ziliisha jana
Say goodbye joto, Rest in Peace Shida
Knock, knock money

RAP:
Wenyewe wanasema usawa unakaba
Na rafiki wa kweli ni mama na baba
Hawa wengine wala usiwaamini
Maana binadamu wa sasa wana roho saba
Watakuwa na wewe kwenye raha
Na hawatakuwa na wewe kwenye njaa
Bora nipige misele yangu peke yangu
Niruke kivyangu na woga niliukataa
Aaah!! Nabadilika kama saa
Na Siku hazigandi na sitokataa tamaa
Wamejaa, usaliti na chuki
Watu wa karibu wanageuka mamluki
Jenero nasonga iwe joto au baridi naamini tutashinda
Kama mbwai iwe mbwai barida
We make more money rest in peace shida
Ukinuna unataka tunune wote
Ukilia unataka tulie wote
Vita vyako tunapigana wote
Tukishinda tushinde au bora tufe wote
Kama kulima kote tumelima wote
Hata kupanda kote tumepanda wote
Kupalilia tumepalilia wote
Aaaargggh !!! nashangaa sasa mbona hatuvuni wote??

Chorus:
Hili joto hasira, ambaa
Upepo hakuna
Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa.
Foleni njia nzima, ambaa
Na pesa hakuna

Ambaa, naruka mwenyewe
Yelela, yelela, ambaa
MWISHO