MWANAMUZIKI mtata katika tasnia ya muziki Afrika
Kusini, Kelly Khumalo, amepata aibu ya mwaka baada ya polisi kumtoa katika
tamasha mjini Soweto na kumhoji kwa shambulio.
Khumalo alikuwa anasakwa na Polisi wa Kituo cha Hillbrow,
mjini hapa baada ya kudaiwa kumshambulia mke wa golikipa wa timu za Orlando
Pirates na Bafana Bafana, Senzo Meyiwa kutokana na masuala yanayohusishwa na
mapenzi.
Ofisa mmoja polisi anayefahamu kesi hiyo alisema
ofisa upelelezi na mwenzake mmoja walienda nyumbani kwa wazazi wa Khumalo, Vosloorus
Jumamosi iliyopita mchana lakini hawakumkuta.
Mtoa taarifa wao aliwaeleza kuwa Khumalo anatarajia
kutoa burudani jioni hiyo katika ukumbi wa Jabulani Amphitheatre mjini Soweto.
Ndipo maofisa hao walipoenda eneo hilo lililokuwa limejaa watu na kumkuta
akijiandaa kupanda jukwaani na bendi yake.
Maofisa hao walimwamuru kutoke nje akiwa mbele ya
umati wa mashabiki, na walimtaka awafuate katika gari lao la polisi ambapo
walichukua maelezo yake na kuondoka.
“Polisi
watapeleka maelezo ya mwanamuzidiki huyo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka ili afanye
maamuzi kama ashtakiwe au la. Lakini kwanza watatakiwa kuchukua maelezo ya dada
yake Kelly na Senzo. Kinachowachanganya
wapelelezi ni kitendo cha Senzo kutotoa ushirikiano jambo ambalo linafanya Mandisa
akose haki yake haraka,” alisema mtoa habari.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyoko polisi, Khumalo alimkuta
Meyiwa akizungumza na mkewe, Mandisa, barabarani. Ndipo mwanamuziki huyo
alipoegesha gari lake na kuwafuata.
Inadaiwa Mandisa alienda upande wa abiria na
alijaribu kufungua mlango lakini ukawa umefungwa. Kisha alirudi kwa Meyiwa na
kumtaka afungue mlango, lakini ghafla inadaiwa sasa mdogo wa Khumalo aliyekuwa
amekaa katika gari la msanii huyo alishuka na kuanza kumshambulia Mandisa.
“Mandisa alipata majeraha usoni baada ya Khumalo
ma mdogo wake kumkwaruza kwa makucha yao usoni,” alisema ofisa huyo.
0 comments:
Post a Comment