Thursday, October 3, 2013

Katty Perry Akiri aliwaza Kujiua

Katy Perry helps launch the Volkswagen Jetta in NYC4
MWANAMUZIKI Katy Perry amekiri kuwa alipata mawazo ya kujiua baada ya kutengana na mumewe mchekeshaji, Russell Brand.
Perry ambaye alitengana na mchekeshaji huyo wa Uingereza Desemba 2011 baada ya ndoa yao kudumu kwa miezi 14, alikiri kuwa alikuwa mkiwa na akajikuta akipata maswali kichwani iwapo aendelee kuishi au la.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 28, ambaye sasa ana uhusiano na John Mayer, anazungumzia kutengana na mumewe katika wimbo Ghost na  By The Grace of God ambazo ziko katika lalbamu yake ijayo ya  Prism.
Perry alilieleza Jarida la Billboard kuwa, " wimbo huo ni ushahidi jinsi gani hali ilivyokuwa ngumu wakati fulani. Nilijiuliza, 'je nataka kuvumilia? Je, niendelee kuishi?
Mwanamuziki huyo ambaye albamu yake mpya inatarajiwa kuzinduliwa Oktoba 18, hivi karibuni aliuza jumba lake la kifahari lenye thamani ya Dola za Marekani milioni 6.5 West Hollywood, California, nyumba ambayo alikuwa akiishi na mumewe Russell.

0 comments:

Post a Comment