STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 25 Aprili , 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amezikumbusha Wizara na Idara za Serikali kutekeleza majukumu yake kwa
wakati na kuripoti kwa mamlaka husika ili matokeo yaweze kutolewa kwa
wananchi.
“Hatujifanyii
sisi bali wananchi tunaowahudumia hivyo hatuna budi tufanye kazi kwa
wakati na kutoa taarifa za utekelezaji huo kwa mamlaka husika ili
wananchi waweze kuelezwa matokeo ya utekelezaji huo” Dk Shein
alisisitiza.
Akihitimisha
kikao cha kujadili utekelezaji wa Mpangokazi wa Wizara ya Miundombinu
na Mawasiliano kwa kipindi cha Julai 2013 hadi Machi 2014 Ikulu jana Dk.
Shein alisisitiza umuhimu kwa Wizara na Idara za Serikali kutumia
mamlaka zinazoongoza Wizara na Idara za Serikali kujadili masuala yao na
kuyachukulia hatua.
“Kukutana
na kushauriana ndio njia pekee ya kufanyakazi kwa ufanisi na kutoa
matokeo mazuri” Dk. Shein alieleza na kusisitiza mashauriano kati ya
wizara na Bodi zinazosimamia taasisi za Serikali kuwa ni lazima
yafanyike mara kwa mara na kutoa taarifa katika mamlaka zilizo juu yake.
Dk.
Shein alibainisha kuwa wajibu wa bodi hizo ni kuzisaidia wizara
kusimamia taasisi zilizo chini yake kwa mujibu wa Sheria na taratibu
zilizowekwa hivyo mawasiliano ya mara kwa mara na wizara ni kitu cha
lazima.
“Idara
zinaripoti kwa Wizara na Wizara zinaripoti Baraza la Mapinduzi”alisema
na kusisitiza kuwa huo ndio utaratibu unaopaswa kufuatwa ili shughuli za
Serikali ziweze kufanyika kwa wakati na kwa ufanisi.
Katika
kikao hicho Mhe Rais aliziagiza Wizara za Serikali kuvipatia nyenzo
vitengo vya Ukaguzi wa Ndani kwa mujibu wa mahitaji na uwezo wa fedha
uliopo ili vitengo hivyo viweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu na
kwa uhuru.
Awali akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji Mpangokazi wa Wizara hiyo Katibu Mkuu Dk. Juma
Malik Akil alieleza kuwa katika kipindi husika Wizara yake ilipanga
kutekeleza miradi ya maendeleo 14 inayojumuisha ujenzi wa barabara,
miundombinu ya viwanja vya ndege na bandari pamoja na mradi wa mageuzi
ya mfumo wa taasisi.
Alifafanua
kuwa miradi hiyo imezingatia utekelezaji wa mipango mikuu ya maendeleo
ya nchi ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo 2020, Mkakati wa Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umasikini-MKUZA II, Sera ya Usafiri Zanzibar, Sera
ya TEHAMA na Mpango Mkuu wa Usafiri Zanzibar (Zanzibar Transport
Masterplan 2009).
Kwa
upande wa ukusanyaji mapato, Dk Akil alieleza kuwa hadi mwezi Machi
2014 Wizara yake imeweza kukusanya jumla ya shilingi milioni 306 ikiwa
ni asilimia 75 ya lengo la Wizara hiyo la kukusanya shilingi milioni 406
kwa mwaka wa fedha wa 2013/2014.
0 comments:
Post a Comment