Meneja
wa NMB Mlimani City Bw. Leonard Ngaya (kushoto) akikabidhi sehemu ya
madawati 55 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi ya Makuburi Jeshini Bi. Stella Kaluse (kulia).
Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Mwenyekiti wa Kata ya Makuburi Bw.
Moshi Kaftanyi (katikati) na Meneja wa NMB tawi la University Bw.
Charles Mapunda . Hafla ya Makabidhiano haya yalifanyika hivi karibuni
katika viwanja vya shule hiyo.
Wawakilishi
toka NMB pamoja na uongozi wa shule wakiwa kwenye picha ya pamoja na
wanafunzi baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa
ajili ya kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo. Hafla ya
makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya makuburi jeshini
hivi karibuni.
Hivi
karibuni, Benki ya NMB imeukabidhi Uongozi wa shule ya msingi Makuburi
Jeshini jijini Dar es Salaam msaada wa madawati yenye thamani ya
shilingi million tano. Madawati ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa
madawati katika shule hiyo.








0 comments:
Post a Comment