ALIYEKUWA
Kocha Mkuu wa timu ya Azam FC, Stewart Hall amepata ulaji mpya baada ya jana
kujiunga na Klabu ya Sunderland AFC ya Uingereza akiwa Meneja wa ‘Kidongo
Chekundu Sports Park’ pamoja na Kituo cha Michezo cha Elite Sports Academy
vinavyojengwa Dar es Salaam.
Vituo
vyote hivyo viwili vitakuwa chini ya Kampuni ya kufua umeme ya Symbion Power
inayoshirikiana na klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England, katika masuala mbalimbali
ya ukuzaji wa vipaji vya michezo ambapo moja ya mikakati yake ni kujenga vituo
mbalimbali vya michezo nchini kikiwamo cha Kidongo Chekundu.
Taarifa
kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana Dar es Salaam na Kitengo cha Mahusiano
ya Umma cha Symbion Power, ikimnukuu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Tanzania,
Peter Gathercole, ilisema Hall ambaye ni Mwingereza amesaini mkataba na kampuni
hiyo bila kueleza ni wa muda gani.
“Stewart
Hall, kocha wa soka Mwingereza, atajiunga na Symbion Power, kampuni kubwa ya
kuzalisha umeme nchini, Sunderland AFC kutoka Uingereza, na Wizara ya Habari,
Utamaduni, Vijana na Michezo, kama Meneja wa Kidongo Chekundu Sports Park
pamoja na Elite Football Academy katika Jiji la Dar es Salaam,” ilisema taarifa
ya Ofisa Mtendaji Mkuu huyo wa Sympion Power Tanzania.
Aidha,
ilimnukuu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC, Margaret Byrne akisema:
“Tumefurahishwa kuona mradi wa kituo cha michezo unaokwenda kwa kasi. Uteuzi wa
Stewart ni maendeleo ya kusisimua na tunajiandaa kuona juhudi kubwa kwa kila
moja anayehusika ili kuleta matunda katika siku za usoni.”
Akizungumza
jana Dar es Salaam, Hall alisema: “Mradi huu utaboresha haraka ubora wa
wachezaji chipukizi katika ngazi ya klabu na timu za Taifa. Chipukizi
watafundishwa masuala ya kiufundi, mbinu, kimwili na mahitaji ya kiakili katika
soka ya kisasa.
“Kutakuwa
na programu iliyosheheni ya ukocha. Nimefurahishwa kuhusu fursa ambazo
zitaletwa kwa ajili ya Watanzania. Wachezaji bora watapewa fursa ya kunolewa
katika Kituo cha Michezo cha Sunderland Academy of Light nchini Uingereza.”
Hall
mwenye leseni ya ukocha ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na kuwa Mkufunzi wa
shirikisho hilo, alikuwa Kocha Mkuu wa Azam FC hadi kumalizika kwa mzunguko wa
Ligi Kuu ya Bara, Novemba 7, mwaka huu walipoachana na klabu hiyo kwa
makubaliano ya pamoja.
Amewahi
kuifundisha timu ya soka ya Taifa ya Zanzibar, na pia ni aliwahi kuwa
Mkurugenzi wa Kituo cha Soka cha timu ya Birmingham City ya Uingereza. Pia
amewahi kufundisha soka akiwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Saint Vincent na
Grenadines pamoja na Pune FC ya India na Sofapaka ya Kenya.
Baada
ya kuachana na Azam FC, minong’ono ilienea katika duru za soka nchini kwamba
anakwenda katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwa Mkurugenzi wa Ufundi,
jambo linalothibitika kuwa si kweli.
Kwa
upande wake, Ofisa Mtendaji wa Sympion Power Tanzania, Gathercole alisema mradi
wa Kidongo Chekundu Sports Park, utakuwa wazi kwa watu wote ambao watakuwa
wanacheza soka katika uwanja wenye nyasi bandia usiku pamoja na viwanja vidogo
vitano, vya umri maalumu.
Kituo
hicho kitakuwa na vyumba vya kubadilishia nguo, chumba cha madaktari chenye
vifaa vya kisasa na mgahawa. Gathercole alisema ujenzi wake utaanza mwezi huu.
Hivi
karibuni, Serikali kupitia kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk Fenella Mukangara ilitangaza kujengwa kwa kituo hicho, hatua iliyotokana na
matunda ya ziara ya Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wake katika kituo cha soka
cha Sunderland, England, Juni mwaka huu.








0 comments:
Post a Comment