IDADI ya wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) imeongezeka kutoka 164,708 hadi kufikia 536,829 kati ya Julai 2012 na Juni 2013.
Mkurugenzi
wa Takwimu na Uhai wa wanachama wa Mfuko huo, Michael Mhando aliueleza Mkutano
wa wadau wa NHIF na CHF mjini hapa juzi kuwa ongezeko hilo ni sawa na asilimia
69.3.
Aidha,
Mhando alisema idadi ya wanufaika
imeongezeka kutoka 691,774 hadi kufikia 2,963,296 kwa kipindi hicho hicho.
Taarifa
ya utekelezaji wa shughuli kuu za mfuko huo
hadi kufikia Juni mwaka huu
inaonesha Sh milioni 202 zikiwa ni michango ya wanachama zilikusanywa
ikilinganishwa na Sh milioni 11.3 zilizokusanywa Julai 2002 mfuko huo
ulipoanzishwa.
Mhando alisema ili kumudu gharama za shughuli
za uendeshaji, mfuko umekuwa ukiwekeza ziada ya fedha kwenye vitega uchumi vya
muda mfupi kama vile amana za Serikali, za benki na hisa.
“Mfuko
unaruhusiwa kisheria kuwekeza ziada baada ya kutoa fedha za madai, shughuli za
uendeshaji wa Mfuko na gharama za maendeleo ya Mfuko” aliwafahamisha washiriki
wa Mkutano huo.
Kutokana
na uwekezaji huo, alisema, zaidi ya Sh milioni 55.8 zilizalishwa hadi kufikia
Juni mwaka huu ikilinganishwa na Sh milioni 38 zilizopatikana mwaka jana.
“Fedha
za uwekezaji zimeendelea kuwa chanzo muhimu kwa mfuko kuendesha shughuli
mbalimbali wakati michango ya wanachama inatumika kulipia huduma za matibabu,”
alisema.
Mkurugenzi
huyo alisema mfuko unagharimia matibabu yote kwa wanachama wake isipokuwa
upasuaji wa urembo, gharama ya tiba kwa madhara ya ulevi au dawa za kulevya na
za tiba kutokana na madhara ya kutaka kujiua au kujinyonga.
Alitaja changamoto zinazoukabili mfuko ni
pamoja na kutopatikana huduma zote ambazo mfuko unazitoa katika baadhi ya vituo
vyenye hadhi ya kutoa huduma hizo.
Pia
upo upungufu wa dawa na baadhi ya wanachama na watoa huduma kutokuwa waaminifu.
Wilaya
ya Chemba yaanza kuunda vikundi vya vijana








0 comments:
Post a Comment