Monday, November 25, 2013

"Niungineshi kununua vifaa vya elimu"

MWANAMITINDO Flaviana Matata ameyataka makampuni,mashirika pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ya elimu kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji maalumu.

Flaviana hivi majuzi alitoa misaaa ya madaftari 800 pamoja na kalamu 800 kwa wanafunzi wa shule ya msingi Minazini iliyopo Mwananyamala.
Flaviana aliyasema hayo wakati akizungumzia harakati zake za kuchangia elimu kwa kuwanunulia vifaa vya shule wanafunzi wenye uhitaji maalum.

Alisema kuwa wapo wanafunzi ambao wanashida hasa katika suala zima la kupata vifaa vya shule kama vile kalamu, madaftari, mabegi na huduma nyingine muhimu.

Alisema kuwa ili kukabiliana na changamoto ni vema makampuni yakajitokeza kuungana mkono na harakati zake katika kuwahudumia wanafunzi.

"Kupitia Taasisi yangu ya Flaviana Matata Foundation kwa sasa tunajihusisha na utoaji wa vifaa vya shule ili kuwasaidia wanafunzi wenye uhitaji maalum hapa nikiwa namaanisha kuwa wanafunzi ambao wazazi wao hawana fedha za kuwanunulia vifaa vvya shule au hata wale ambao ni yatima wanatakiwa kulelewa"alisema Flaviana.

Flaviana aliyakaribisha makampuni kuwanunulia wanafunzi hao vifaa vya shule kupitia Taasisi yake hiyo na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa wamechangia pia fedha za kusaidia harakati nyingine za kijamii.

Aliongeza kuwa vifaa vya shule vina nembo ya jina la Taasisi yake na kwa kampuni itakayonunua bidhaa za kusaidia wanafunzi kupitia kwake itatajwa pia katika vifaa hivyo.


0 comments:

Post a Comment