
MBUNIFU mahiri wa mavazi nchini
Sheria Ngowi amesema kuwa kwa sasa anatarajia kufungua maduka ya kazi zake
nchini Kenya, Nigeria na Afrika Kusini ili kuongeza idadi ya wateja wake.
Ngowi ambae kwa sasa anasifika zaidi
kutokana na umahiri wake wa kushona suti nzuri kwa staili tofauti huku akiwa
amewavalisha watu mbalimbali maarufu hapa nchini.
Akizungumza na safu hii alisema kuwa
ubunifu ni soko ambalo linatakiwa kufanyiwa uwekezaji wa hali ya juu kwa kuwa
kwa sasa wau wengi wanapenda kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa ndani.
Alisema kuwa katika nchi hizo
kutakuwa na wawakilishi wake ambao watakuwa wakisikiliza mahitaji ya wateja na
kisha kufanyiwa kazi.
Alisema kuwa analenga kuhakikisha
kuwa kila mtu anavaa nguo zilizobuniwa naye.
Alisema kuwa atahakikisha kuwa iwapo
mtu asipovaa suti inayotengenezwa naye basi atavaa tai, suruali au hata shati
lenye kubuniwa na yeye.
Aliongeza kuwa suti yake moja
anashonesha kwa kuanzia milioni hadi milioni nne na tano.
"Mimi kwa sasa nina mikakati ya
kuhakikisha kuwa ninaongeza soko langu katika ubunifu na kuongeza wateja ikiwa
pamoja na kuwakilisha watanzania katika sekta ya ubunifu nchini"alisema
Ngowi.








0 comments:
Post a Comment