TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, amezindua rasmi Kiwanda cha Kusindika Chai cha Ikanga, Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, amezindua rasmi Kiwanda cha Kusindika Chai cha Ikanga, Tarafa ya Lupembe, Wilaya ya Njombe katika Mkoa Mpya wa Njombe.
Kiwanda hicho kinachomilikiwa kwa asilimia 25 na wakulima wa
chai wa Lupembe ni ukombozi mkubwa wa wakulima wa Tarafa ya Lupembe ambao
wamekuwa wanakabiliwa na ukosefu wa sehemu ya kuuza chai yao.
Ufunguzi wa kiwanda hicho cha Ikanga Tea Factory
kinachomilikiwa na Kampuni ya Ikanga Tea Factory Limited ni utekelezaji wa
ahadi ya Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete
wakati anafanya kampeni ya Urais katika Tarafa ya Lupembe mwaka 2010. Ni
kiwanda kipya zaidi na bora zaidi cha kusindika chai katika Tanzania.
Ujenzi wa kiwanda hicho ulianza mwishoni mwa mwaka 2010
baada ya Serikali ya Rais Kikwete Mei mwaka huo huo kuiomba Kampuni ya Mufindi
Tea and Coffee Limited (MTC) kujenga kiwanda cha kusindika chai ya wakulima
ambayo sehemu yake kubwa ilikuwa inapotea na kuoza kwa sababu ya ukosefu wa
kiwanda.
Ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho, MTC iliunda kampuni
mpya ya Ikanga Tea Company Limited Septemba 2010. Kampuni hiyo ni ubia kati ya
MTC na wakulima wa chai wa Lupembe ambao wanamiliki asilimia 25 za hisa za
kiwanda hicho kupitia umoja wao wa Lupembe Tea Farmers Trust.
Uzinduzi wa leo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa kiwanda
hicho. Chini ya awamu hiyo ya kwanza yenye uwezo wa kusindika tani 1,800 za
chai kwa mwaka kwa kutumia njia moja ya uzalishaji iliyokamilika Juni
mwaka jana kwa gharama ya Sh. bilioni 3.75. Awamu ya pili ambayo
inaendelea kujengwa, itagharimu Sh. bilioni 1.48 na ikikamilika kiwanda
kitakuwa na uwezo wa kusindika tani 3,500 na awamu ya tatu na ya mwisho
itagharimu Sh.bilioni 1.5 na kukamilika kwa awamu hiyo kutakiwezesha kiwanda
kusindika tani 5,000 za chai kwa mwaka.
Chini ya uendeshaji wa Kiwanda hicho, chai yote ya wakulima
inanunuliwa kwenye vituo maalum na kusafirishwa kwenda kiwandani na magari ya
Kiwanda. Wakulima pia wanapewa mbolea kwa mkopo na wakulima wote wa chai
inayochukuliwa na kiwanda hulipwa kila mwezi kwa bei iliyopangwa na Bodi ya
Chai Tanzania.
Miongoni mwa mipango ya Kampuni ya Chai ya Ikanga ni kununua
angalau hekta 600 za ardhi ili nayo ianze kulima chai ili kuongeza kiwango cha
chai kinachozalishwa katika eneo la Lupembe na ukamilishaji wa shule kwa ajili
ya watoto wa wakulima wa eneo la Lupembe.
Rais Kikwete amezindua Kiwanda hicho ikiwa ni shughuli ya kwanza katika shughuli nyingi ambazo atazifanya wakati wa ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Njombe kuzindua na kukagua shughuli za maendeleo. Miongoni mwa shughuli hizo itakuwa ni kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe.
Rais Kikwete amezindua Kiwanda hicho ikiwa ni shughuli ya kwanza katika shughuli nyingi ambazo atazifanya wakati wa ziara yake ya siku sita katika Mkoa wa Njombe kuzindua na kukagua shughuli za maendeleo. Miongoni mwa shughuli hizo itakuwa ni kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2013
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2013








0 comments:
Post a Comment