7:00 AM

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Msanii Azma amejibu maswali ya mashabiki wake.....soma hapo alivyandika kwenye ukarasa wake.
JE WANASUBIRI NIFE-NI DISS KWA NEY WA MITEGO NA CLOUDS FM?
Tangu nimeachia video mpya ya wanasubiri nife, nimepata simu nyingi
siku ya leo, na wengi wananiuliza kama hii nyimbo nimeandika kwa ajili
ya kumdiss Ney wa Mitego na clouds fm? Kutokana na mistari ifuatayo
''najua mnajua kuwa mnajua, ila hamuwezi nichukua kwenye tour,
mnawachukua wasiojua. mitego wanayotega naitegua, ingawa wachache
wanabana, ninafanya, ninafana na kupiga hatua''
JIBU
Huu wimbo nimeandika mahususi kwa watu wote, ambao wanajifanya hawaoni
umuhimu wangu, wakati nafsi zao zinajua fika kuwa mimi ni bora zaidi ya
hao ambao wanawafanya waonekane bora ,sikuandika kwa lengo la kumdiss
NEY au Clouds fm ila kama mistari Imewagusa na maandiko yangu
yametafsirika hivyo ni furaha kubwa sana kwangu, hicho ni kitu ambacho
mwandishi yeyote anatamani iwe hivyo,kwa kuwa hadi mnatafsiri maanake
mnajadili, endeleeni kujadili ili sanaa yetu ikue..
NB
SHUKRANI KWA WOTE MNAO SHARE NA KUENDELEA KUSHARE VIDEO YANGU HII MPYA
facebook,kwenye page zenu, blogs na website zenu au kucheza audio ya huu
wimbo,shukrani sana kwa BONGO5 kwa uchambuzi wenu maana ndio umepelekea
watu wengi kunipigia simu,nina hakika watu wote wangekuwa wanafuatilia
kama nyinyi hii sanaa ingefika mbali sana
MUNGU AWABARIKI WOTE.......
AZMA/THE AFRICAN AMBASSODOR/TAMADUNI MUZIK
0 comments:
Post a Comment