
MKURUGENZI wa soka wa
Barcelona, Andoni Zubizarreta amesisitiza kwamba mshambuliaji wao, David Villa
anayewaniwa na Arsenal hatauzwa, kwani si utaratibu wao kuwauza wachezaji wao
bora katikati ya msimu.
Mchezaji huyo wa
kimataifa wa Hispania amekuwa akipigania kupata namba kwenye kikosi hicho,
tangu alipopona majeraha ya mguu wake aliovunjika na sasa amehusishwa na mpango
wa kuondoka klabuni hapo Januari.
Arsenal imekuwa ikitajwa
kwamba inawania kumsajili Villa wakati wa dirisha dogo la usajili Januari,
lakini sasa Barcelona imebainisha wazi kwamba haitamuuza.
“Januari tutaendelea kuwa
na Villa na vizuri kuelewa kwamba Barcelona haina utaratibu wa kuwauza
wachezaji wake bora wakati wa dirisha dogo la Januari,” amesema Zubizarreta
akiiambia televisheni ya Canal Plus.
“David ni mchezaji ambaye
analeta mabao kwa timu, hivyo hatuna sababu ya kumuuza.
“Na sasa amepona kabisa
baada ya kuvunjika mguu na naamini kwamba sasa atarudi dimbani akiwa na ari
kubwa mno ya kufunga mabao.”
0 comments:
Post a Comment