
ANDREY
Arshavin ameripotiwa kwamba atauzwa kwa pauni milioni 4 kwenda klabu ya
Reading, wakati wa dirisha dogo la usajili Januari.
Arsenal
imemruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Urusi kuzungumza na klabu hiyo iliyopo
mkiani mwa Ligi Kuu ya hapa na anatarajia kukamilisha taratibu zote wiki ya
kwanza ya Januari.
Washika
bunduki hao wameshafikia makubaliano na Reading juu ya ada na imeripotiwa
kwamba atauzwa kwa pauni milioni 4.
Vyanzo
vya habari vimeithibitishia tovuti ya goal.com kwamba, Arshavin ameshaichezea
Arsenal mechi yake ya mwisho na anaondoka hapo wiki ya kwanza wakati wa dirisha
dogo la usajili litakapofunguliwa.
Arsene
Wenger ameruhusu kuuzwa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31, ambaye
hajaanza katika mchezo wowote msimu huu tangu alipoaanza kwenye mchezo wa Ligi
ya mabingwa Ulaya Desemba 4 mwaka huu dhidi ya Olympiakos.
Awali
klabu za Fulham na Zenit St Petersburg ambayo ni timu ya zamani ya Arshavin,
zilikuwa zinawania saini yake, lakini sasa Reading ndiyo imeweza kumtwaa nyota
huyo.
0 comments:
Post a Comment