Wednesday, September 26, 2012

PAH ONE WAFUNGUKA KUHUSU KUKUTWA NA SILAHA

Wasanii wa kundi la Pa 1 wamekamatwa na silaha walizokuwa wakizitumia kwenye shooting ya filamu yao inayohusu maisha tofauti ya vijana mtaani. Member wa PA 1 `Ola ' alisema tukio hilo limetokea mida ya jioni walivyokuwa wakitoka kwenye shooting ya Movie hio walikutana na Askari maeneo ya Sinza ,wakasachiwa na kukutwa na silaha hizo. Kabla ya kupata nafasi ya kujieleza na kabla askari kutambua kuwa zilikuwa  silaha feki na zakuigizia tu PA 1 walijikuta chini ya ulinzi kituoni.  Baada ya kukaa kituoni kwa saa chache waliweza kutoa maelezo kamili kuhusu silaha hizo na kupata uongozi wa PA 1 ndio wakatolewa kwa dhamani .

PA 1 wametaka mashabiki zao waelewe kuwa kilichotokea sio kitendo kibaya ila nikutoelewana tu na kwa sasa wapo nje kwa dhamana mpaka watakapo maliza jambo hilo na Polisi .Fahamu kuwa filamu wanayo fanya PA 1 inahusu maisha ya Gangsters mitaani ,Maisha ambayo wa
tu wengi hawajapitia. Demo ya filamu hio itatoka siku yoyote.

Baada ya Inteview kwenda hewani Kupitia Power Jams ,Ola Aliandika Hivi Kwenye FaceBook.

0 comments:

Post a Comment