Showing posts with label Kinana. Show all posts
Showing posts with label Kinana. Show all posts

Monday, December 9, 2013

KINANA AMALIZA ZIARA, APANDA TRENI YA TAZARA KUREJEA DAR.ALAKIWA KWA SHANGWE

 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha Rose Migiro wakiteremka kwenye Treni ya Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) Stesheni ya Mlimba, mkoani Morogoro jana, tayari kwenda kuwasalimia wafuasi wa CCM pamoja na wananchi wakiwa safarini kutoka Makambako mkoani Njombe kwenda Dar es Salaam. Kinana na msafara wake walikuwa katika ziara ya siku 26 katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njomba kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM.
 Kinana na Nape wakimwangalia Dk. Migiro akiteremka kwenye treni hiyo katika Stesheni ya Mlimba.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwa na Katibu wa CCM Kata ya Mlimba Selemani Balali  wakati msafara wa Kinana ulipoteremka kwa muda katika Stesheni ya Mlimba.

 Nape akiangalia samaki waliokuwa wakiuzwa katika stesheni la Mlimba, Kulia ni Dk. Migiro.
 Kinana, Migiro na Nape wakiwa na baadhi ya viongozi wa CCM Kata ya Mlimba alipotembelea Stesheni ya Mlimba.
 Komredi Kinana akiwa na Katibu wa CCM,Kata ya Mlimba Selemani Balali  alipokuwa akielekea kupanda treni katika Stesheni ya Mlimba, Morogoro kwenda Dar.
 Kinana akizungumza na baadhi ya wananchi katika Stesheni ya Mlimba
 Jopo la wanahabari wa Televisheni, magazeti, Redio na mitandao ya Kijamii (Bloggers), walioambatana na msafara wa Komredi Kinana  wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili salama katika Stesheni ya Dar es Salaam leo asubuhi.
 Kinana akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida baada ya kuwasili salama katika Stesheni ya Dar es Salaam leo asubuhi.
 Dk. Migiro akilakiwa na Madabida
 Nape akikukbatiwa kwa furaha na madabida ya kuwasili Dar es Salaam  leo.
 Kinana akivalishwa skafu na Chipukizi alipowasili Dar es Salaam leo.
 Komredi Kinana, Nape Nnauye  na Dk. Migiro wakiwasalimia wafuasi wa CCM waliofika kuwalaki katika Stesheni ya Tazara, Dar es Salaam.
 Komredi Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM
 Dk. Migiro na Nape wakiimbiwa wimbo
 Madabida akihutubia wakati wa mapokezi hayo
 Nape akiwashukuru wanahabari waliombatana nao kwenye msafara katika ziara ya siku 26 katika mikoa minne.
 Kinana akihutubia na kutoa shkurani kwa mapokezi hayo pamoja na wanahabari alioambatana nao kwenye ziara hiyo, akiwemo mmiliki wa Blogu hii ya Kamanda wa Matukio, ambaye pia ni Mpiga Picha Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda.
 Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kulia) akiwa miongoni mwa wanaCCM waliofika kuulaki msafara wa Kinana.
 Kinana akiwashukuru wanahabari alioambatana nao kwenye ziara hiyo.
 Kinana akimkumbatia mtangazaji wa Redio Uhuru, Sheila Simba
 Nape akikukmbatiana na Mhariri wa Habari wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe
Kinana akimkumbatia mwandishi wa Kituo cha Televisheni cha Star, Joseph Mpangala. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA Blog ya Kamanda wa Matukio.

Wednesday, December 4, 2013

Kinana ahaidi kusaidiana na Mwakyembe kumaliza kero za Tazara

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jijini Mbeya.Kinana alisikiliza kero mbalimbali kutoka kwa uongozi pamoja na wafanyakazi ambapo aliahidi kusaidiana na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzipeleka ngazi za juu kuzijadili.

Mfanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, Herry Mutashobya akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani), kuhusu hujuma mbalimbali zinazofanyiwa Tazara. Jumla ya kero 35 aliambiwa Kinna na wafanyakazi hao.
 Mfanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, Gerald Simiko akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (hayupo pichani), ambapo alilalamikia kitendo cha uongozi wa mamlaka hiyo, kuwatesa wanaostaafu kwa kutowapatia stahili ya mafao yao wanapostaafu kazi. Kinana alifanya mkutano huo wa kusikiliza kero za wafanyakazi hao katika Stesheni ya Mbeya leo.
 Kinana akihutubia katika mkutano huo na wafanyakazi
 Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ambaye pia ameteuliwa na Rais kuwa Mbunge, Asha Rose Migiro (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, D, Mary Mwanjelwa wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana, katika Kijiji cha Iwambi, Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM wakati wa mapokezi katika Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
 Kinana akitoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa Tazara, Mbeya  leo.
 Kinana akizungumza na wanachama wa CCM waliofika kumlaki katika Kata ya IwambiMbeya Mjini.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwa na Kada wa CCM, Charles Mwakipesile wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana katika Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
NAPE akiwa amekaa na baadhi ya wananchama wa Shina namba 7 la CCM Iyunga, Mbeya Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Monday, December 2, 2013

KINANA ATINGA WILAYA YA MBARALI LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi, eneo la Igawa, wilyani Mbarali, Mbeya.
 Kinana akihutubia wakati wa mapokezi hayo, Kinana na msafara wake walikuwa wanatokea Chunya mkoani humo.
 Kinana akikata utepe kuzindua jengo la ofisi za CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali leo.
Jengo jipya la CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali.PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

Monday, November 18, 2013

KINANA AWAUNGURUMIA WATENDAJI WA VYAMA VYA MSINGI USHIRIKA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA.

 Ndugu Kinana na Ujumbe wakienda kukagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto,kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh.Vita Kawawa,Katibu wa NEC,Siasa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa Wodi ya Wazazi na Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  wakishiriki kuchanganya sementi kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto inayojengwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.
 Jengoo la Utawala wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo.
 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake walipokuwa wakikagua majengo ya hospitali  hiyo.
 Barabara ya kuelekea kwenye hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa ameongozana na Ujumbe wake wakipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha kufua Umeme ndani ya Wialaya ya Namtumbo. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifungua shina la Wakereketwa la Waendesha Bodaboda Wilayani namtumbo,Kinana aliwachangia vijana hao kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya benki,ili waweze kupata mikopo  ya kununua piki piki kwa ajili ya shughuli zao.
Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wa Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wanancho hao walikwenda mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
21
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.Vita Kawawa amewatuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na Ofisa Ushirika wa mkoa huo wa kuwambambikizia madeni wakulima wa Tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea,ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na Wananchi kuachiwa mzigo mkubwa wa kulipa madeni ambayo hayawahusu,hali inayowapelekea wakulima hao kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Mchomoro Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma mara baada kupokelewa vyema na wananchi ya Wilaya hiyo ya Namtumbo.
 Mbunge wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro Wialayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata chai nyumbani kwa balozi wa shina,Said Husein mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama na kukagua uhai wa chama katika mkoa wa Ruvuma.