Showing posts with label CCM. Show all posts
Showing posts with label CCM. Show all posts

Friday, May 9, 2014

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU WILAYANI IGUNGA LEO.


 Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu,Injinia Makoye Luhuya akielezea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbutu kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo,wilayani Igunga mkoani Tabora
 Ujenzi wa daraja la Mbutu ukiendelea kwa kasi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiweka mbao wakati wa ujenzi wa daraja hilo ukiendelea,wilayani Igunga mkoani Tabora mapema leo asubui.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja hilo,Injinia Makoye Luhuya kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (mbele) akishuka, baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. 
 Sehemu ya Daraja hilo Mbutu kama lionekanavyo pichani.

Wednesday, December 18, 2013

WAZAZI WAMALIZA SEMINA MOROGORO

 KATIBU wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa, akizungumza na washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, mwishoni mwa semina hiyo, Des 18, 2013. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Charles Mgonja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge.
 Washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, wakiwa katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013, wakati wa semina hiyo.
 Katibu Mwenezi wa CCM, mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba akizungumza na washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, mwishoni mwa semina hiyo, Des 18, 2013. Wengine kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya ya Kinondoni, Charles Mgonja, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni Salum Madenge na Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa. Kushoto ni Katibu wa Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage.
 Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Abilah Mihewa (kulia) akiingia ukumbini kujumuika na  washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013.
 Washiriki wa semina ya Viongozi wa Jumuia ya Wazazi wilaya ya Kinondoni, wakila kiapo cha kuyashika mafunzo, walipokuwa kwenye semina hiyo, katika ukumbi wa Road View, mkoani Morogoro, Des 18, 2013
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akimshukuru Katibu wa Itikadi na Uenezi, CCM mkoa wa Morogoro Dorothy Mwamsiku baada ya Katibu huyo kufungua semina ya viongozi wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Wilaya ya Kinondoni, katika ukumbi wa Road View mkoani Morogoro, Des 17, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

Tuesday, December 10, 2013

TAMKO LA WENYEVITI WA CCM-MIKOA

TAMKO LA WENYEVITI WA CCM-MIKOA LA KUMPONGEZA KATIBU MKUU WA CCM NDG. ABRAHAMANI KINANA NA SEKRETARIETI  YA CCM TAIFA.
 LEO TAREHE 10/DESEMBA/2013
OFISI NDOGO YA CCM DAR- ES- SALAAM
Sisi Wenyeviti wa CCM-Mikoa tuliokutana leo Tarehe 10/Desemba/2013 hapa Dar es salaam, kwa kauli moja na kwa niaba ya wanaCCM wa mikoa yetu, tunatoa kauli ya kumuunga mkono Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi ndugu Abrahamani Kinana na Sekretarieti yote kwa utekelezaji uliotukuka wa majukumu yao ya kichama. Tangu alipopewa wadhifa wa Ukatibu Mkuu ameonyesha uwajibikaji mkubwa, uliokiwezesha Chama kupata uhai mpya na kuamsha Ari na matumaini zaidi ya Watanzania kwa Chama Cha Mapinduzi.
WanaCCM nchini tuko katika mstari wa mbele kuisimamia Serikali yetu kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 sura ya Tisa; Inayokitaka Chama kuisimamia Serikali yake. 
Kwa pamoja tunaungana na kupinga kwa nguvu zote mambo yafuatayo;
1.      Ubadhirifu unaofanywa katika Serikali za Mitaa nchini unaozifanya Halmashauri nyingi kujirudiarudia kupata hati chafu na zenye mashaka, inayosababisha hasara na manung’uniko kwa wananchi.
2.      Utelezaji duni wa baadhi ya miradi ya maendeleo unaopelekea kuwepo kwa huduma duni na zisizokidhi thamani ya fedha na matakwa ya kitaalamu. Hii inaashiria uwepo wa Rushwa na ubadhirifu wa fedha kwa baadhi ya miradi ya maendeleo.
3.      Ucheleweshaji wa maslahi na stahiki za watumishi wa Umma kunakopelekea kuwa wavunja moyo na ari watumishi, katika kutekeleza majukumu yao na hivyo kusababisha kutokea kwa migomo ya mara kwa mara kufuatia uzembe katika kuwapatia haki zao, kinyume na misingi ya utawala bora.
4.      Gharama kubwa ya uendeshaji wa shughuli za Serikali na Taasisi zake ikilinganishwa na gharama zinazotumika kwenye miradi ya maendeleo na uboreshwaji wa huduma za jamii kwa wananchi.
5.      Usimamizi mbovu wa Operation mbali mbali za Serikali zenye nia njema kwa Taifa. Mfano Operasheni kuhamisha wafugaji na Operasheni Tokomeza; Zina nia njema lakini usimamizi wake umekuwa mbovu hata kupelekea kuvuruga nia yake njema kwa Taifa.
6.      Kushindwa na Kuchelewa kutatua baadhi ya Kero sugu kwa Wananchi kama malalmiko mbali mbali ya wakulima (mfano mbolea za minjingu kutofanya vizuri kwa asilimia kubwa, matatizo ya wakulima wa pamba na korosho nk.) na wafugaji; Rushwa zilizokithiri katika sehemu mbali mbali za utoaji wa huduma kwa wananchi na ucheleweshwaji wa fadha za miradi ya maendeleo nk.
Katibu Mkuu wa CCM daima amekuwa akikemea kwa nguvu zote madhaifu yote tuliyoyataja hapo juu na sisi kama Wenyeviti wa CCM Mikoa yote Tanzania. Tunaitaka Serikali ichukue hatua za haraka katika kurekebisha madhaifu hayo. Viongozi na watendaji wengine wote wa Serikali, walioonesha udhaifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao, na ambao walipewa wito na wengine ambao wanatakiwa kupewa wito; wa kuhudhuria mbele ya Kamati Kuu ya CCM wachukuliwe hatua zinazostahili. Tunawakumbusha viongozi wa Serikali watambue kuwa Chama cha Mapinduzi kinaisimamia Serikali kwa mujibu wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-2015 Sura ya Tisa.
_______________________________________________
Mgana Izumbe Msindai – Mwenyekiti  wa Wenyeviti Mikoa

______________________________________________________
Haji          Juma  Haji – Makamu Mwenyekiti  Wa Wenyeviti Mikoa

______________________________________________
Lucas Ole Mukusi – Katibu wa Wenyeviti  Mikoa

TUNAWASILISHA

Monday, December 2, 2013

KINANA ATINGA WILAYA YA MBARALI LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na wafuasi wa CCM wakati wa mapokezi Igawa, alipoanza ziara ya kuimarisha uhai wa chama katika Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya asubuhi leo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) akiwasalimia wananchi wakati wa mapokezi, eneo la Igawa, wilyani Mbarali, Mbeya.
 Kinana akihutubia wakati wa mapokezi hayo, Kinana na msafara wake walikuwa wanatokea Chunya mkoani humo.
 Kinana akikata utepe kuzindua jengo la ofisi za CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali leo.
Jengo jipya la CCM Tawi la Ihanga, wilayani Mbarali.PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA

Monday, November 18, 2013

KINANA AWAUNGURUMIA WATENDAJI WA VYAMA VYA MSINGI USHIRIKA NA BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI MKOANI RUVUMA.

 Ndugu Kinana na Ujumbe wakienda kukagua ujenzi wa jengo la Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto,kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo.
Pichani kulia ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh.Vita Kawawa,Katibu wa NEC,Siasa Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro wakishiriki katika ujenzi wa msingi wa Wodi ya Wazazi na Watoto katika hospitali ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma.

 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa pamoja na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana  wakishiriki kuchanganya sementi kwa ajili ya ujenzi wa Wodi ya Wazazi ya akina mama na Watoto inayojengwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Namtumbo kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete.
 Jengoo la Utawala wa hospitali hiyo ya wilaya ya Namtumbo.
 Pichani shoto ni Mbunge wa jimbo la Namtumbo,Mh Vita Kawawa akimuongoza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake walipokuwa wakikagua majengo ya hospitali  hiyo.
 Barabara ya kuelekea kwenye hospitali hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa ameongozana na Ujumbe wake wakipata taarifa ya mtambo wa kufua umeme katika kituo cha kufua Umeme ndani ya Wialaya ya Namtumbo. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akifungua shina la Wakereketwa la Waendesha Bodaboda Wilayani namtumbo,Kinana aliwachangia vijana hao kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwafungulia akaunti ya benki,ili waweze kupata mikopo  ya kununua piki piki kwa ajili ya shughuli zao.
Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa wa Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Lwinga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Namtumbo kwenye uwanja wa Taifa mkoani Ruvuma.Ndugu Kinana na ujumbe wake wapo kwenye ziara ya kikazi mkoani Ruvuma,Mbeya na Njombe katika kukagua Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama cha CCM,kusikiliza matatizo ya Wananchi ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiletea maendeleo. Katika Ziara hiyo ya Tunduru na Namtumbo wananchi wamelalamikia kuhusu bei ya zai la Korosho na Tumbaku,kama vile haitoshi wanancho hao walikwenda mbali zaidi kwa kulalamikia suala zima la Mbolea.
21
Mbunge wa Jimbo la Namtumbo Mh. Vita Kawawa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Namtumbo, mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Taifa.Vita Kawawa amewatuhumu baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika na Ofisa Ushirika wa mkoa huo wa kuwambambikizia madeni wakulima wa Tumbaku kupitia ruzuku ya mbolea,ambapo makadirio ya mbolea inayohitajika kwa wakulima huongezwa kinyemela na Wananchi kuachiwa mzigo mkubwa wa kulipa madeni ambayo hayawahusu,hali inayowapelekea wakulima hao kutokuwa na imani na baadhi ya viongozi wa chama na serikali.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa kata ya Mchomoro Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma mara baada kupokelewa vyema na wananchi ya Wilaya hiyo ya Namtumbo.
 Mbunge wa jimbo la Namtumvo,Vita Kawawa akifafanua jambo kwa Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,Dkt.ASharose Migiro pamoja na Katibu wa NEC Siasa,Itikadi na Uenezi,Nnape Nnauye ndani ya Kata ya Mchomoro Wialayani Namtumbo mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu wa CCM,ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata chai nyumbani kwa balozi wa shina,Said Husein mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mchomoro wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.Kinana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama na kukagua uhai wa chama katika mkoa wa Ruvuma.

Tuesday, September 17, 2013

NAPE: CHADEMA WAWEWESEKA

  

CHADEMA WAWEWESEKA!
  ~.Ni baada ya Kinana kupeleka neema ya wakulima wa pamba(soko na bei).
~. Ujenzi wa viwanda Shinyanga wawapa homa
~. Ajira kwa vijana kuwakosesha Chadema waandamanaji.
~. Waishia kumparamia balozi wa China
~. Kinana: tuna deni la kuwatumikia wananchi sio kulumbana.

Kasi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha 2010/2015 imeibua kiwewe kwa vyama vya upinzani hasa Chadema. Kiwewe hicho kimedhihirishwa na shutuma za Chama hicho kwa balozi wa China nchini kwa uamuzi wa nchi hiyo kuwekeza kwenye viwanda vya pamba na mazao yatokanayo na mifugo kwa mkoa wa Shinyanga.

Katika mkutano wa Chadema na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Chadema walidai kitendo cha Balozi wa China Dk. Lu Youqing kushiriki katika mkutano wa hadhara wa CCM mjini Shinyanga ni cha utovu wa nidhamu, uvunjifu wa sheria hoja ambazo hazina mashiko.

Hata hivyo Katibu wa NEC ya CCM itikadi na uenezi Ndg. Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari kijijini Mwandoya, wilayani Meatu mkoa wa Simiyu kwenye ziara ya Katibu mkuu wa CCM mkoani humo aliwataka watanzania na wanakanda ya ziwa kuzipuuza shutuma hizo dhidi ya balozi wa China na akawataka waendelee kuunga mkono juhudi za CCM za kutekeleza ilani yake ya uchaguzi.

"tatizo la hawa Chadema wamezoea kufanya harakati zao kwa kutumia matatizo ya watu, sasa leo juhudi za CCM kutatua tatizo la bei ya pamba na soko lake inawanyang'anya mtaji wao muhimu sana ndo maana wanapiga kelele. Lakini pia tatizo la ajira kwa vijana wao walikua wanalitumia kama mtaji wa kupata waandamanaji, sasa vijana wakipata ajira kwenye viwanda hivi ambavyo vitaanza kazi Desemba mwaka huu, watakosa waandamanaji ndio chanzo cha kelele zote hizi" alisisitiza Nape

Nape alisisitiza kuwa vyama vyote vya siasa vina vyama rafiki kutoka nchi mbalimbali duniani, lakin tofauti inakuja kwenye aina ya urafiki husika, na kutoa mfano wa tofauti ya urafiki kati ya Chama Cha Kikomunisti cha China na CCM kuwa umelenga katika shughuli za maendeleo, lakini kwa upande wa Chadema ni tofauti.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Kinana amekuwa akisisitiza mara kadhaa kuwa CCM ina deni kubwa la kuwatumikia wananchi katika kutimiza ahadi zao kwa wananchi walizozitoa kupitia ilani ya uchaguzi ambayo watanzania waliichagua mwaka 2010 na ahadi mbalimbali za wagombea wa CCM.

"sisi CCM tuna kazi ya kuwatumikia wananchi,kutimiza ahadi zetu kwao na sio kulumbana na wapinzani. Na hii ndio tofauti ya chama kilicho madarakani na vyama vya upinzani, wakati wao kila kukicha wanatafakari wazungumze nini sisi tunahangaika kuwatumikia wananchi waliotupa dhamana ya kuongoza nchi yetu.

Tuesday, August 27, 2013

DADA WA FREEMAN MBOWE AJIUNGA NA CCM, ARUDISHA KADI YA CHADEMA

Picture: Grace MboweDADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za 
kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
Picture: Grace Mbowe, Hassan Mtenga
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. 
Source HabariLeo