Grace
amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata
hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu
ya familia.
Alikabidhi
kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za
kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale
pale.
Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za
kuwadanganya wananchi.
Alisema
itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake
siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.
“Nimeamua
kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka
Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na
kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani
upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.
Alisema,
“kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa
kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo
wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”
“Freeman
Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia
CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo
jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za
upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment