Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na
wafanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni
ya Mbeya, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua
miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya
Uchaguzi ya CCM jijini Mbeya.Kinana alisikiliza kero mbalimbali kutoka
kwa uongozi pamoja na wafanyakazi ambapo aliahidi kusaidiana na Waziri
wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kuzitafutia ufumbuzi kwa kuzipeleka
ngazi za juu kuzijadili.
 |
| Mfanyakazi wa
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni ya Mbeya, Herry
Mutashobya akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
(hayupo pichani), kuhusu hujuma mbalimbali zinazofanyiwa Tazara. Jumla
ya kero 35 aliambiwa Kinna na wafanyakazi hao. |
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (Tazara), Stesheni
ya Mbeya, Gerald Simiko akizungumza mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana (hayupo pichani), ambapo alilalamikia kitendo cha
uongozi wa mamlaka hiyo, kuwatesa wanaostaafu kwa kutowapatia stahili ya
mafao yao wanapostaafu kazi. Kinana alifanya mkutano huo wa kusikiliza
kero za wafanyakazi hao katika Stesheni ya Mbeya leo.
Kinana akihutubia katika mkutano huo na wafanyakazi
Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, ambaye pia ameteuliwa na Rais
kuwa Mbunge, Asha Rose Migiro (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Viti
Maalum Mkoa wa Mbeya, D, Mary Mwanjelwa wakati wa mapokezi ya msafara wa
Kinana, katika Kijiji cha Iwambi, Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
 |
| Kinana akisalimiana na wanachama wa CCM wakati wa mapokezi katika Kata ya Iwambi, Mbeya Mjini leo. |
Kinana akitoka baada ya kuzungumza na wafanyakazi wa Tazara, Mbeya leo.
Kinana akizungumza na wanachama wa CCM waliofika kumlaki katika Kata ya IwambiMbeya Mjini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwa na Kada wa CCM,
Charles Mwakipesile wakati wa mapokezi ya msafara wa Kinana katika Kata
ya Iwambi, Mbeya Mjini leo.
NAPE akiwa amekaa na baadhi ya wananchama wa Shina namba 7 la CCM Iyunga, Mbeya Mjini.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
0 comments:
Post a Comment