Showing posts with label Entertainment News. Show all posts
Showing posts with label Entertainment News. Show all posts

Saturday, September 20, 2014

PICHA: Petit Man afunga Ndoa Na Dada Yake Diamond Platnumz ‘Esma Platnum’

Meneja wa Mirror na wasanii wa Endless Fame Petit amethibitisha kuwa na mapenzi ya ukweli kwa Esma kwa kufunga nae ndoa kama ilivyoripotiwa mapema.Hii piccha na ujumbe kutoka kwa Petit.
petit 3petit 2Wema Alipost ujumbe huu kwaajili yao
Wat can I say…. Im super happy for you two…. Wenyewe mlianza kimasihara maskini…. Who would ve known dat itafika hii siku and now mmehalalishwa…. Wow….!! Proud of u toto and to you my beautiful Esma, I wish u nothing but happiness…. Nawapenda sana… and nawatakia kila lililo lenye khery… Mpendane na muheshimiane katika maisha yenu ya ndoa… Ndoa ni baraka na naomba mwenyezi mungu awafungulie kila kulipofungwa na awatie ujasiri…. muishi kwa amani na upendo hadi pale kifo kitakapowatenganisha…. dah hadi machozi yamenitoka.
petit 4petit 7petit 8petit 9

Saturday, May 31, 2014

T.I AMTUMIA UJUMBE MZITO BONDIA MAYWHEATHER, ASEMA YUPO TAYARI KWENDA JELA

Floyd Mayweather Jr. Hosts Party At MGM's Studio 54
T.I na Floyd Money Maywheather
Tangu kutokea kwa ugomvi  baina ya  Rapa T.I na Bondia Floyd Maywheather kwenye mgahawa wa Fatburger  mjini Vegas, hali bado si shwari,  huku kila upande ukijaribu  kutoa majigambo kufuatia ukaribu uliokuwepo kati ya mke wa T.I  na bondia huyo asiyekuwa na rekodi ya kupigwa hata pambano moja tangu aanze kupigana ngumi za kulipwa.
Kutoka katika mtandao wa Instagram, kiongozi huyo wa kundi la Hustle Gang alikaririwa akisema alifanya vile kwa ajili ya familia yake na kisha kupost picha   iliyoambatana na ujumbe uliotafsiriwa   huenda ukawa unamlenga  moja kwa moja Maywheather   kutokana na wawili hao kuwa katika uhasama.
“I’ll Ride,Die,Steal,Kill,Do Life in a Jail fad a fam…. If it mean that much to u…proceed. If not Stand Down… Simple.” aliandika T.I na kisha kupost picha akiwa na familia yake kama inavyoonekana hapo chini.
TroubleMan31

Thursday, May 22, 2014

NEWS: Hii ndiyo website ya Gosby itakayozinduliwa hivi karibuni

Kupitia facebook page yake msanii anayefanya poa, Gosby ameweka link ya website yake atakayoizindua siku za karibuni .
unaweza kutembelea hapa ili upate taarifa pindi itakapoanza Gosbymusic

Friday, May 9, 2014

Apple kuinunua kampuni ya Dr Dre ‘Beats Electronics’ kwa dola bilioni 3.2!

Dr Dre kuwa billionaire wa kwanza mwanamuziki, apple yanunua kampuni yake kwa dola billion 3, Diddy akubali kufunikwa


Kampuni ya Apple imepanga kuinunua kampuni ya Dr. Dre ya ‘Beats Electronics’ inayotengeneza bidhaa ya headphones maarufu za ‘Beats by Dr Dre’ na imepanga kumlipa dola billion 3.
Malipo hayo yatamfanya Dr Dre kuwa sio tu mwanamuziki tajiri zaidi duniani lakini pia mwanamuziki wa kwanza kuwa Billionaire.
Kwa mujibu wa Finance Times, endapo Apple watanunua kampuni hiyo kwa dola billion 3.2 itakuwa imefanya manunuzi yenye thamani zaidi ya kuinunua kampuni nyingine.
Mchongo huu utamfanya Dr. Dre kuupiku utajiri wa P.Diddy ($ 700 Million) zaidi ya mara tatu kwa kuzingatia kuwa Diddy ndiye rapper mwenye pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa akifuatiwa na Dr Dre kwa mujibu wa Forbes.
Kupitia Instagram, Puff Daddy ameandika ujumbe wa kumpongeza Dr Dre na kuonesha kuwa sasa inabidi aongeze bidii ‘time to go to work’.
“This is BIG! This is Historical! If anyone deserves it, it's you! Congratulations Dr. Dre! #fromthesoontobe #DrCombs #wemadeit #proudofyou #thebarhasbeenrsised #motivated #timetogotowork.” Puff Daddy ameandika kwenye Instagram na kuambatanisha picha ya Dr Dre..

Saturday, May 3, 2014

Adam Mchomvu ndani ya game ya muziki Rasmi, atazindua video mbili na wasanii kibao akiwemo Juma Nature, Fid Q kushikilia nafasi ya Mchomvu (MC)

Mtangazaji wa kipindi cha XXL na Bongo Fleva ya Clouds Fm, Adam Mchomvu a.k.a Baba Jonni,siku ya juma pili anatarajia kudondosha mzigo wa video za nyimbo zake mbili ndani ya Maisha Club.
Licha ya wimbo wake wa Jonny kunfanya aonekane zaidi kwa upande wa Muziki, Mchomvu atazindua video mbili, ikiwa ni ya Au Sio  na Una Akili wewe. vido ambazo zimefanya na kampuni mbili tofauti moja ikiwa imesimamaiwa na HK, na nyingine imesimamiwa na Benjamin wa Mambo Jambo.

"Baada ya watu wengi kujua game ninayofanya, na wengi wao kuona kama siko serious, ndio maana kwa sasa nimeamua kuingia katika Mziki kwa miguu yote miwili..." amesema Adam
Mchomvu atazindua video hizo akiwa na wasanii  kibao  kama T.I.D, County Boy, Chege, Juma Nature, KCK, Mirror, Dogo Asley, Godzilla, Weusi na wengineo, huku Kwenye Mc wa show hiyo akiwa ni Fid Q

Tuesday, April 8, 2014

WASHINDI 3 BORA WA SHINDANO LA KUSAKA VIPAJI VYA UIGIZAJI TANZANIA ( TANZANIA MOVIE TALENTS) KANDA YA ZIWA KUPATIKANA LEO

Majaji wa Shindano la Kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents, Single Mtambalike (kulia), Yvonne Chery (Katikati) na Roy Sarungi (Kushoto) wakipitia alama za washiriki kwaajili ya kuweza kuwatangaza washindi waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo wanachukuliwa washiriki 30 kwaajili ya kupata mchujo wa washindi watatu bora ambao wataibuka na Kitita Cha Shilingi laki 5 kila Mmoja kwa Kanda ya Ziwa na baadae kujiunga na washindi wengine watatu kutoka kila kanda katika fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na Mshindi Kujinyakulia Zawadi Kubwa kabisa ya Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania. (50,000,000/=)
 Baadhi ya washiriki wakionyesha uwezo wao wa kuigiza mara baada ya kupewa muswada (script).
Baadhi ya washiriki wakiwa mbele ya majaji (hawapo pichani) kwaajili ya kutajwa washiriki waliofanikiwa kuingia hatua ya tatu ambapo washiriki 30 tu ndio watachukuliwa kwaajili ya kupatikana washindi watatu watakaoibuka na kitita cha Shilingi laki 3 kila Mmoja na Baadae kuungana na washindi wengine wa kanda zilizobakia katika Fainali ya mwisho itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wawili (wa kwanza kulia na wapili) wakiwa hawaamini kama wamechaguliwa kuingia hatua ya washiriki 30 kwaajili ya mchujo wa kupata washindi watatu wa Kanda ya Ziwa, Mkoani Mwanza
 Mmoja wa washiriki aliyefanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu (mwenye fulana nyeupe) akipongezwa na mshiriki mwenzie ambae hakupata bahati ya kuchaguliwa kwaajili ya kuendelea na hatua inayofuata.
 Washiriki wakipongezana mara baada ya kuchaguliwa kuendelea na hatua inayofuata.
Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kuchaguliwa kwa hatua ya tatu wakishangilia mara baada ya kuchaguliwa.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Mwanza

Sunday, April 6, 2014

50 Cent Thanks Eminem For Giving Him A Shot, Describes Him As One Of His Favorite People

50 Cent Thanks Eminem For Giving Him A Shot, Describes Him As One Of His Favorite People

50 Cent remains grateful for the opportunity Eminem provided him, and counts him among his favorite humans.

In case you hadn't noticed, it's been a slow news day, folks. As such, we thought we'd bring this moment of homage to light, given Ferrari F's recent departure from Aftermath Entertainment and Interscope / Shady Records.
Fif took to Instagram yesterday and posted an image of himself in the studio with Eminem, accompanied by the following caption: "I traveled a lot of places. Met a lot of people. But EM is my favorite. He gave me my shot, man. That's all I needed. I ran with it." (This was followed by the obligatory #SMSAUDIO hashtag, of course.) Check out the post in the gallery above, if you wish.
It's good to know these two are still on good terms, especially with 50's proposed comeback on the horizon. His new album Animal Ambition is slated to drop on June 3rd, and so far we've heard "Pilot", "Don't Worry Bout It", "Hold On" and "Smoke", his latest single, which you can listen to below. Trey Songz contributes to the hook and offers a verse of his own as well, the

Saturday, April 5, 2014

Na hii ndiyo official logo ya PKP kutoka kwa @ommydimpoz

2 
Omari Nyembo ambaye jukwaani anaitwa Ommy Dimpoz, zaidi ya muziki pia ni mjasiriamali akitumia kampuni yake ya PKP ambayo huwa inaandaa show pamoja na kutoka mavazi yenye logo hiyo.
Ommy ametoa logo rasmi ya kampuni yake ambayo rangi ya dhahabu imetumika sana kwenye logo hiyo kama inavyoonekana hapa.
1 
Credit: Millard Ayo

Friday, April 4, 2014

Albamu ya 2pac ndiyo inaongozwa kwa kuwa na lugha chafu kuliko zote Duniani

Tarehe 1 April 2014 Best New Ticket imefanya utafiti kugundua album ipi ina maneno machafu zaidi toka mwaka 1985 mpaka mwaka 2013 na kugundua kuwa album ya marehemu  2 Pac ‘All EyeZ On’ ndio album inayoshika namba moja kwa maneno na lugha chafu zaidi.
Utafiti huu umeangalia album 2,296 za muziki wa rap zilizotoka kuanzia mwaka 1985 mpaka mwaka 2013. zinazochaguliwa kwa mauzo bora, ukubwa wa jina la msanii na jinsi album ilivyopokelewa na wateja sokoni.
Album mbili za Tupac, 2Pacalypse ya mwaka 1996 na All Eyez On Me imekutwa na lugha chafu ikiwaimetumika mara 901, matusi ni asilimia 33.52 kwenye wimbo mmoja na neno Nigger likitajwa mara 404. Asilimia 44 ya matusi kwa album yote.
Kweney All Eyez On Me yenye cd mbili na nyimbo 27 nayo ina lugha chafu zaidi, Album ya Notorious B.I.G. Ya mwaka 1997 ‘Life After Death’ yenye nyimbo 23, lugha chafu imetumika mara 615, matusi ni asilimia 26.73 kwa wimbo mmoja.

kundi la Mafikizollo kuwasili leo jijini Dar


Kundi maarufu la muziki wa Kwaito la nchini Afrika kusini, Mafikizolo linatarajia kutua mchana huu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya onesho moja tu linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City, kesho, Jumamosi Aprili 5 mwaka huu.

Mafikizolo imekuwa na rekodi nzuri ya kushinda kwenye tuzo mbalimbali za muziki, kutokana na kupiga muziki na kucheza kwa umahiri, hasa mtindo wao maarufu wa Kwaito.

Kundi hilo linaloundwa na wasanii wawili(Nhlanhla Nciza na Tebogo Madingoane pichani juu), kwa sasa linalotamba na vibao kama "Khona" na "Happiness", watawasili nchini kesho mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini.

Akiongea na gazeti hili, mratibu wa onyesho hilo Vinny Magere kutoka kampuni ya Juegacassa, amesema Mafikizollo, wanatarajia kufanya onesho moja tu maalum na la kihistoria litakalodumu kwa muda wa saa nne.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa kundi hili kufika nchini, tangu kuachia wimbo wao wa "Khona", wimbo ambao umesababisha kundi hilo kujizolea umaarufu mkubwa kwenye kumbi za starehe, na hata katika vituo mbali mbali vya redio.

Mafikizolo kwa sasa wanashikilia taji la kundi bora la mwaka, kwa mujibu wa tuzo za muziki za SAMA (South African Music Awards), huku wakiongozwa kwa kutajwa mara nyingi  kwenye tuzo za Ulaya kama kundi bora la muziki kutoka Afrika.

Kundi hilo maarufu kuliko yote yaliyowahi kutokea kusini mwa Afrika liliwahi kutamba pia miaka ya nyuma na nyimbo kama "Ndihamba Nawe", "Ndixolele", "Sebenza", "Ndashata" na "Ndizolila".

Onesho la hilo, linatarajiwa kuanza saa moja usiku ambapo kiingilio kitakuwa shilingi 20,000 kwa watakaolipa kabla ya onyesho, huku mlangoni watalipia shilingi 35,000 za kitanzania.

Kundi hilo mwaka huu, limeingia katika vipengele vinne kwenye kinyanga’anyiro kikubwa cha tuzo za SAMA.

Katika kinyang’anyiro hicho chenye vipengele 28, kundi hilo limepata nafasi ya kuwania vipengele vinne, ambavyo ni Kolabo Bora ya Mwaka, albam Bora ya Pop ya Mwaka, albam ya Mwaka kupitia albam ya Reunited, na kundi  bora la Mwaka.

Kwa mujibu wa tovuti ya destinyconnect, hafla ya ugawaji tuzo hizo itafanyika nchini humo Aprili 28 mwaka huu.

Kundi hili lilianza shughuli za kimuziki tangu miaka ya 1990, albamu yao ya kwanza walitoa mwaka 1996. Tangu hapo wameshatoa albamu sita, baada ya kutoa albamu yao ya tano mwaka 2003 "Kwela". 

Kundi lilianza kutetereka na baadaye mwaka 2013 waliungana tena na kutoa albamu ya sita iliyoitwa "Reunited" na kutoa singo yao ya kwanza "Khona" wimbo ambao umewatambulisha upya.

Thursday, April 3, 2014

Ushindi wa Lupita Nyong’o wachochea sekta ya Filamu Kenya

Bado waafrika na wakenya wanaendelea kusheherekea ushindi wa Lupita Nyong’o, katika tuzo za Oscar kwa kuwa mwigizaji bora msaidizi katika filamu ya “Twelve years a Slave”.
Ushindi huo umesisimua watengenezaji wa filamu nchini Kenya na kuwapa matumaini ya kuwa, kupitia vipaji vyao wanaweza kutambulika kama vile Lupita.
Gavana wa jimbo la Machakos nchini humo ameanzisha kituo cha kutengeneza filamu, kukuza vipaji vya watengenezaji filamu pamoja na burudani, maarufu kama Machawood, kituo kitakacho kuwa cha aina yake barani Afrika.
SOMA ZAIDI: SAMMISAGO.COM

Friday, March 14, 2014

MABIBO BEER YA WADHAMINI BONGO MOVIE KUADHIMISHA MIAKA MITATU TANGU KUANZISHWA KWAKE


Rais wa Bongo Movie, Steve  Mengele  ‘Steve Nyerere' (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maadhimisho ya miaka mitau tangu kuzaliwa kwa Bongo Movie yatakayo fanyika Machi 28 katika ukumbi wa East 24 Arcade  uliopo Barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limeted. Kutoka kushoto ni Devotha Mbaga, Claud Issa na Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Calvin  Costa.
Viongozi wa Bongo Movie wakiwa kwenye mkutano huo.
Ofisa Mauzo wa Kampuni ya Mabibo, Calvin  Costa akitoa taarifa kwa ufupi kuhusu udhamini walioutoa kwa Bobo Movie.

Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira (kulia), akitoa hutuba fupi katika mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

UONGOZI wa Bongo Movie jana umetangaza tarehe ya  kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa  itakayoadhimishwa kwa shamrashamra mbalimbali Machi 28   watakapoaadhimisha miaka mitatu tangu kuzaliwakatika ukumbi wa East 24 Arcade  uliopo Barabara ya Mwai Kibaki Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Rais wa Bongo Movie Steve  Mengele almaarufu kwa jina la ‘Steve Nyerere’alisema  kwamba  siku hiyo kutakuwa na  burudani ya aina yake kutoka kwa bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Kadhalika Nyerere aliwatangaza wadhamini ambao wataghariamia sherehe hiyo kuwa ni kinywaji cha Windhoek.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisa mauzo wa kanda ya kinondoni Calvin  Costa aliongeza  kwa kusema siku hiyo kinywaji hicho cha Windhoek ndicho kitakachonyweka.

“Tunawaita mashabiki na wadau wake kwa wingi siku ya sherehe hiyo ambayo tuna matumainui sisi kama wadhamini itaacha gumzo la aina yake” alisema  Costa.

Akitoa neno la shukran Jackline Wolper aliongeza kwa kuwashukuru Windhoek kwa kuwadhamini mwaka huu kwani miaka yote wamekuwa wakijichangisha ili kufanya sherehe hiyo.

Mweka Hazina wa Bongo Movie  Issa Musa ‘Cloud amesema kwamba kutakuwa na  zulia jekundu ambapo mashabiki wataweza kupiga picha na wasanii bila usumbufu siku hiyo huku akisistiza kuwa tiketi zitauzwa kabla, kwa sh.10,000 na meza sh. 50,000.

Wakati huohuo kutakuwa na shindano kwa wasanii waliopita na kutwaa taji la Miss Tanzania huku mshindi akiondoka na zawadi ya aina yake kutoka Windhoek.

Picha za Oscar Pistorius akiwa na damu zaonyeshwa mahakamani

0314-oscar-pistorius-01
Picha za Oscar Pistorius alizopigwa na polisi muda mfupi baada ya kumpiga risasi mpenzi wake, zimeonyeshwa mahakamani kama ushahidi.
Picha hizo zinamuonyesha bingwa huyo wa zamani wa Olimpiki akiwa amesimama kwenye damu huku akiwa amevaa kaptura  ambayo ina damu.
Mapema katika wiki hii Pistorius alitapika mahakamani baada ya mwanapatholojia kuelezea jinsi majeraha ya mateso aliyoyapata mpenzi wa Pistorius, Reeva Steenkamp, baada ya kumpiga risasi katika siku yake ya mwisho wa wapendanao.

Tazama picha nyingine akitapika ndani ya mahakama.