Friday, March 14, 2014

Picha za Oscar Pistorius akiwa na damu zaonyeshwa mahakamani

0314-oscar-pistorius-01
Picha za Oscar Pistorius alizopigwa na polisi muda mfupi baada ya kumpiga risasi mpenzi wake, zimeonyeshwa mahakamani kama ushahidi.
Picha hizo zinamuonyesha bingwa huyo wa zamani wa Olimpiki akiwa amesimama kwenye damu huku akiwa amevaa kaptura  ambayo ina damu.
Mapema katika wiki hii Pistorius alitapika mahakamani baada ya mwanapatholojia kuelezea jinsi majeraha ya mateso aliyoyapata mpenzi wa Pistorius, Reeva Steenkamp, baada ya kumpiga risasi katika siku yake ya mwisho wa wapendanao.

Tazama picha nyingine akitapika ndani ya mahakama.

0 comments:

Post a Comment