Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas
Mwakibinga akiwaonesha waandishi wa habari uthibitisho wa malipo ya shilingi
milioni 400 ikiwa ni sehemu ya pili ya malipo kwa ajili ya Ligi Kuu.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Azam Media Rhys
Torrington (kulia) akimkabidhi Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania Silas Mwakibinga nakala ya uthibitisho
wa malipo ya fedha kwa ajili ya Ligi Kuu ya Vodacom.
KAMPUNI
ya Azam Media imetangaza kuwa tayari imeshatuma fedha kwa Bodi ya Ligi
kwa ajili ya msimu wa ligi wa Vodacom kwa mwaka 2014/ 2015.
Fedha
hizo zimetolewa mapema zaidi kwa ajili ya kusaidia maandalizi mapema
kwa timu kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba wa miaka mitatu ya udhamini
wao katika ligi hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana katika ofisi za Azam zilizopo Tazara, Dar
es salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Rhys Torrington, alisema
kuwa kampuni hiyo inavutiwa na aina nzuri ya ushirikiano kati yake na
bodi ya Ligi.
Alisema
kuwa kupitia bodi hiyo Azam imepiga hatua kubwa katika kufanikisha
adhma yake ya kuifanya Ligi hiyo ya Vodacom kuwa ya kuvutia zaidi.
“Ligi
hii tunataka kuifanya kuwa ni moja kati ya ligi zinazovutia na kuonesha
ushindani barani Afrika, ingawaje ninajua kuwa kuna mengi ambayo
yanatakiwa kuendelea kufanywa ili kuipa nguvu zaidi ligi hii”alisema
Torrington. Alisema
kuwa kwa kutambua hilo ndio maana Azam Media imehakikisha kuwa klabu
zote zinapata fedha mapema ili kusaidia suala zima la maandalizi.
Akizungumzia
mikakati ya baadae ya Azam Media alisema kuwa inatarajia kuanza
kuonesha soka la mitaani (street soccer) mbalimbali moja kwa moja (live)
itakayokuwa ikiendelea kwenye nchi za Kenya na Uganda.
Alisema
kuwa kwa sasa Azam Media imeanza kujikita katika nchi za Kenya, Uganda
na Malawi ambapo itakuwa ikiuza ving’amuzi vyake katika nchi hizo. Aliongeza
kuwa pia katika kuhakikisha kuwa inatoa mwanya zaidi wa vipindi vizuri
na vya kuvutia inaendelea na vipindi vya michezo vya Morning Trumpet,
sport@8 pamoja na Kwetu House.
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi, Mr Silas Mwakibinga
alisema kuwa kwa hatua hiyo ya Azam ya kuhakikisha upatikanaji wa fedha
hizo kwa wakati ni nzuri na itasaidia kuzipatia timu muda mzuri wa
kujiandaa. Alisema
kuwa bodi yake inavutiwa sio tu na utangazaji wa vipindi unaofanywa na
Azam bali pia hata nia yao ya kuendeleza soka la Tanzania.
Azam Media ilisaini mkataba wa miaka mitatu na wenye thamani ya TSHS5,560,800,000 kuonesha mechi za live na za kurekodi mechi za Ligi Kuu na fedha hizo zinalipwa kwa awamu tatu.







0 comments:
Post a Comment