Tuesday, May 13, 2014

VIDEO:Wasanii wa Bongo Movie Mzee Majuto na JB wakiongelea safari yao ya UTURUKI

Uongozi wa Uturuki pamoja na wasanii wa filamuUongozi wa Princess Casino na Wasanii
Wasanii hao ambao amepata udhamini Princess International Casino wamesema safari hiyo ya wiki moja wataitumia kwenda kujifunza mambo mbalimbali yatayowasidia kukuza sanaa yao. Akizungumza na waandishi wa habari akiwa Princess Casino ndani ya IT Plaza Jijini Dar es salaa, mmoja kati ya wasanii hao,Jacob Stephan amesema kuwa wameahidiwa na Princess International Casino kwenda kukutana na watu muhimu kwenye tasinia yao.
“Princess Casino wametuahidi kule tutakutana na watu muhimu sana kwenye shughuli ambayo tunafanya,kwangu mimi naiita hii ni fursa kwasababu ni vitu ambavyo tulikuwa tunaomba,” alisema. 
 
Pia kwa upande wake mchekeshaji mkongwe King Majuto amedai kuwa katika safari hiyo atajifunza na kuangalia tamaduni za watu wa Uturuki.
“Mimi nimefurahi sana kwenda Uturuki,huu ni mwanzo mutasikia Majuto kahamia Uturuki, safari yangu ni kujua utamaduni wao,mimi nimefarijika sana kwenda kubadilisha mawazo kwa mapuMziko. Hii ni heshima kubwa sana kwangu haswa,kwasababu niliganda hapa mpaka nafa, leo nimepata faraja ygingine tena isije ikaniua,” alisema. 

0 comments:

Post a Comment