MWENGE wa Uhuru ulioingia wilayani Temeke juzi, ulitarajiwa
kuzindua miradi 12 yenye thamani ya Sh bilioni 19 wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kupokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema alisema
ni faraja mwenge huo unapoendelea kukimbizwa na kuzindua miradi kwani inaonesha
jinsi Serikali inavyowajali wananchi wake.
Mjema alisema miradi iliyotarajiwa kuzinduliwa na mwenge huo
itawawezesha wananchi wa Temeke kupunguza adha waliyokuwa wakipata kutokana na
kukosa baadhi ya mahitaji.
"Mwenge unapoendelea kuwaka inaonesha jinsi Serikali
inavyowajali wananchi wake katika shughuli mbalimbali ikiwemo za maendeleo,
Watanzania ni mashahidi katika hili," alisema Mjema.
Awali Mkuu wa Wilaya ya Ilala, alisema katika wilaya yake
mwenge huo umezindua jumla ya miradi tisa ambayo imegharimu Sh bilioni 2.2.
Mwenge huo unatarajiwa kulala katika viwanja vya Zakhem, Mbagala kabla ya
kukabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi.
0 comments:
Post a Comment