Sunday, June 23, 2013

Prandelli Aomba Radhi kwa kumuita Balotelli Mweusi

 
KOCHA wa Italia  Cesare Prandelli ameomba radhi kwa kusema kuwa Mario Balotelli ni mchezaji pekee aliyeruhusiwa kutoka nje ya hoteli Brazil kwa sababu ni mweusi.
Maofisa ulinzi walikiambia kikosi hicho kwamba hawaruhusiwi kutoka nje ya hoteli wakati huu wa michuano ya Mabara.
Prandelli alisema mshambuliaji huyo wa  AC Milan aliruhusiwa kutoka nje ya hoteli kwa sababu: "rangi yake ni tofauti na yetu,". Lakini baadaye akasema: "Samahani, ilikuwa ni utani".
Ilikuwa ni lazima atoke kwa sababu mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City Balotelli alitakiwa kwenye hafla ya hisani kusaidia watoto waishio kwenye mazingira magumu wa Salvador.
Awali tukio hilo ilikuwa lifanyike Rio lakini ilibadilishwa na kuhamishiwa hapa, mahali ambapo tuliambiwa hakuna anayeruhusiwa kutoka mbali na hoteli".
"Kabla sijazungumza lolote kuhusu rangi ya ngozi... napenda kuweka wazi sababu za yeye pekee kuruhusiwa kutoka nje ya hoteli".
"Alitoka, lakini hakuwa na kazi nyingine ya kufanya zaidi ya kushiriki kazi ya hisani kwa ajili ya watoto hao".
Italia jana usiku ilitarajiwa kucheza na wenyeji Brazil kwenye Kombe la Mabara, mechi iliyotarajiwa kuwa ya vuta nikuvute.
mwisho.

0 comments:

Post a Comment