
Lulu
aliwasilisha maombi ya dhamana kupitia kwa jopo la mawakili wake, Kennedy
Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe kwa kuwa shitaka linalomkabili
linadhaminika.
Maombi
hayo yaliwasilishwa chini ya hati ya dharura, wakitaka yasikilizwe na kuamriwa
mapema kwa madai kuwa mshitakiwa amekaa rumande kwa muda mrefu.
Akisoma
uamuzi huo jana, Jaji Zainab Mruke alisema kuwa, mahakama imekubali ombi hilo
la dhamana kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake
ya msingi.
Alisema
Lulu atakuwa nje kwa dhamana endapo atakuwa na wadhamini wawili, wafanyakazi wa
serikali watakaosaini hati ya Sh milioni 20, atatakiwa kuwasilisha hati zake za
kusafiria kwa msajili wa mahakama na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila
idhini ya Msajili wa Mahakama.
Aidha
anatakiwa kuripoti mahakamani kila mwezi hadi kesi yake ya msingi
itakapokwisha, pia Jaji Mruke alisema ingawa dhamana ni haki yake kisheria
lakini ikumbukwe kuwa kuna roho ya mtu imepotea hivyo lazima sheria zifuatwe.
Alimtaka
msajili wa mahakama kuhakikisha masharti yote yanatimizwa na kuongeza kuwa:
“Mshitakiwa ataendelea kubaki rumande hadi atakapotimiza masharti hayo.”
Baada
ya kuambiwa dhamana yake imekubaliwa Lulu alianza kulia mahakamani, hata hivyo
alirudishwa rumande kwa kuwa hakutimiza masharti ya dhamana baada ya kuchelewa
kuwasilisha hati yake ya kusafiria kwa msajili wa mahakama.
Awali
Wakili Kibatala aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mshitakiwa kwa masharti
ambayo itaona yanafaa kwa kuwa shitaka linalomkabili Lulu lina dhamana, ambapo
upande wa mashitaka haukuwa na pingamizi.
Kesi
hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa
na mashitaka ya kumuua Kanumba kwa kukusudia hata hivyo baada ya upelelezi
kukamilika, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) alibadilisha mashitaka dhidi yake na
kuwa ya kuua bila kukusudia.
Baadaye
ilihamishiwa Mahakama Kuu na kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia,
lenye namba ya usajili 125 ya mwaka jana na kupangiwa kusikilizwa mbele ya Jaji
Zainab Mruke. Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza
Vatican, alimuua Kanumba bila kukusudia.
0 comments:
Post a Comment