Showing posts with label Lulu. Show all posts
Showing posts with label Lulu. Show all posts

Tuesday, January 29, 2013

LULU ATOKA MAHABUSU KWA DHAMANA

AKIWA amesota mahabusu kwa takribani siku 274 au  miezi tisa hatia maye Msanii machachari wa filamu nchini Elizabeth Michael “Lulu” anayekabiliwa na mashitaka ya mauaji bila kukusudia ya  Steven Kanumba ametoka mahabusu kwa dhamana. 
Dhamana hiyo ilitolewa jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaama baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyotolewa jna Jaji Zainab Mruke.
Alitimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili wanaofanyakazi serikalini, ambao wamesaini hati ya Sh milioni 20 kila mmoja, amewasilisha mahakamani hati zake za kusafiria, anatakiwa kuripoti mahakamani tarehe mosi ya kila mwezi na kutosafiri nje ya Dar es salaam bila ruhusa ya msajili wa mahakama.
Lulu alifikishwa mahakamani hapo jana saa 7:50 mchana akiwa kwenye gari la polisi lenye namba za usajili STK 2823 na kufikishwa mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam Francis Kabwe kwajili ya kukamilisha taratibu za dhamana. 
Mtuimishi wa Wizara ya Ardhi Florian Mutafungwa pamoja na Dkt Verus Kataruga kutoka Wizara ya Afya ambapo saa 10:00 alitoka chini ya ulinzi baada ya kukamilisha masharti ya dhamana. 
Lulu aliwasilisha maombi ya dhamana chini ya hati ya dharura akiomba yasikilizwe na kuamriwa haraka kwa kuwa amekaa rumande kwa muda mrefu na kosa lake lina dhamana.
Akitoa uamuzi wa ombi la dhamana ya Lulu lililowasilishwa, Jaji Mruke alisema Mahakama imekubali ombi hilo kwa kuwa, shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake ya msingi .
Akizungumza baada ya kupewa dhamana, Lulu aliwashukuru watu wote walikuwa wanamsaidia katika kipindi  chote tangu alipokamatwa hadi anapata  dhamana na kuomba waendelee kumuombea.
“Nawashukuru watu wote lakini naomba muendelee kuniombea kwa kuwa huu ni mwanzo tu kesi hii bado ndio kwanza inaanza” alisema Lulu huku akitokwa na machozi. 
Aliondoka  na gari gari lenye namba za usajili T 480 CFX Kwa upande wake Wakili wa Lulu, Peter Kibatala alisema, dhamana ni mkataba kati ya mshitakiwa na mahakama na kuna taratibu za kufuata ndio maaana walichelea lakini anashukuru msajili kwa kusubiri hata baada ya muda wa kazi kuisha ili Lulu apate halki yake ya msingi.
Lulu alitakiwa kupewa dhamana juzi hata hivyo alirudishwa rumande kwa kuwa alichelewa kuwasilisha mahakamani hati yake ya kusafkiria hadi msajili alipoondoka baada ya saa za kazi kuisha.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa na mmashitaka ya kumuua Kanumba kwa kukusudia hata hivyo baada ya upelelezi kukamilika, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) alimbadilishia mashitaka na kuwa kuua bila kukusudia shitaka ambalo lina dhamana.
Baadaye kesi hiyo ilihamishiwa katika Mahakama Kuu na kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia lenye namba 125 ya mwaka jana, na kupangwa kusikilizwa mbele ya Jaji Mruke. Hata hivyo kesi hiyo bado haijpangiwa tarehe ya kuanza kusikilizwa.
Lulu anadaiwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza Vatican, alimuua msanii Kanumba bila kukusudia.
Baada ya kutoka mahakamani Lulu alipokewa na Mama yake, na wasanii wenzake Dkt Cheni, Abdukarim Kenyata “Mc Kenyata na Muna pamoja na ndugu zake wengine.

Monday, January 28, 2013

Lulu Aachiwa Kwa Dhamana, Lakini Akwama

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuachia kwa dhamana msanii wa Filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' anayekabiliwa na mashitaka ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.
Lulu aliwasilisha maombi ya dhamana kupitia kwa jopo la mawakili wake, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatala na Fulgence Masawe kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika.
Maombi hayo yaliwasilishwa chini ya hati ya dharura, wakitaka yasikilizwe na kuamriwa mapema kwa madai kuwa mshitakiwa amekaa rumande kwa muda mrefu.
Akisoma uamuzi huo jana, Jaji Zainab Mruke alisema kuwa, mahakama imekubali ombi hilo la dhamana kwa kuwa shitaka linalomkabili linadhaminika na dhamana ni haki yake ya msingi.
Alisema Lulu atakuwa nje kwa dhamana endapo atakuwa na wadhamini wawili, wafanyakazi wa serikali watakaosaini hati ya Sh milioni 20, atatakiwa kuwasilisha hati zake za kusafiria kwa msajili wa mahakama na kutosafiri nje ya Dar es Salaam bila idhini ya Msajili wa Mahakama.
Aidha anatakiwa kuripoti mahakamani kila mwezi hadi kesi yake ya msingi itakapokwisha, pia Jaji Mruke alisema ingawa dhamana ni haki yake kisheria lakini ikumbukwe kuwa kuna roho ya mtu imepotea hivyo lazima sheria zifuatwe.

Alimtaka msajili wa mahakama kuhakikisha masharti yote yanatimizwa na kuongeza kuwa: “Mshitakiwa ataendelea kubaki rumande hadi atakapotimiza masharti hayo.”
Baada ya kuambiwa dhamana yake imekubaliwa Lulu alianza kulia mahakamani, hata hivyo alirudishwa rumande kwa kuwa hakutimiza masharti ya dhamana baada ya kuchelewa kuwasilisha hati yake ya kusafiria kwa msajili wa mahakama.
Awali Wakili Kibatala aliiomba mahakama itoe dhamana kwa mshitakiwa kwa masharti ambayo itaona yanafaa kwa kuwa shitaka linalomkabili Lulu lina dhamana, ambapo upande wa mashitaka haukuwa na pingamizi.
Kesi hiyo ilifunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu huku Lulu akikabiliwa na mashitaka ya kumuua Kanumba kwa kukusudia hata hivyo baada ya upelelezi kukamilika, Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) alibadilisha mashitaka dhidi yake na kuwa ya kuua bila kukusudia.
Baadaye ilihamishiwa Mahakama Kuu na kusajiliwa kama shauri la kuua bila kukusudia, lenye namba ya usajili 125 ya mwaka jana na kupangiwa kusikilizwa mbele ya Jaji Zainab Mruke. Lulu anadaiwa kuwa Aprili 7 mwaka jana katika eneo la Sinza Vatican, alimuua Kanumba bila kukusudia.