Mtayarishaji wa
muziki P Funk Majani amefunguka kwa baadhi ya wasanii na wadau wa muziki
kutothamini mchango wake katika muziki wa Bongo Fleva mpaka sasa ulipofika.
Hayo yalisemwa baada
ya kupokea tuzo ya mtayarishaji bora wa muziki wa Tanzania, tuzo ambazo
ziliandaliwa na Baabkubwa Magazin kwa kutambua mchango wake katika tasnia ya
muziki hususani Bongo Fleva
Alisema kuwa wasanii
wengi wameingia katika muziki wa bongo fleva bila kutambua mchango wake katika
muziki huo kitu ambacho hakileti heshima ya Bongo Fleva
"Bila mimi Bongo
Fleva isingekuwepo ila watoto hawatambu mchango wangu wanadharau bila ya kujali
nimeupigania vipi mziki huu mpaka kuufikisha hapa ulipo" alilalamika P
Funk.
Alisema kuwa mchango
wake ni mkubwa katika muziki huo kutofautisha na thamani anayopeka katika
tasnia hiyo pamoja na wadau wa muziki kiujula.
Malalamiko hayo
yametokana na kuwepo na muziki wa Bongo fleva nchini na watu kunufaika na muziki
huo huku wakionekana kusahau mchango wa mtu aliyeibua mziki huo na kuufanya
kuwepo ulipo sasa.







0 comments:
Post a Comment