Hali
ya malkia wa muziki wa kizazi kipya nchini Rehema Chalamila (Ray C) inaendelea
kutengama baada ya kuendelea kupata matibabu na huduma muhimu kwa watu wake wa
karibu akiwemo Ruge Mutahaba.
Akizungumzia
swala hilo Mkurugenzi wa Nyumba ya kukuza Vipaji (THT) Ruge Mutahaba alisema
kuwa hali ya msanii huyo kwa sasa inaridhisha kwa kupatiwa huduma ya karibu
ikiwemo ushauri ili iweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
Alisema
kuwa kwa upande wake yeye anatoa mchango mkubwa kwa msanii huyo ili aweze
kurudi katika hali yake ya kawaida na kuendelea kufanya vizuri katika kazi zake
za muziki.
Ruge
alisema kuwa wasanii wengi wanajikuta wanaingia katika maswala ya ulevi na
kubwia unga kwani inatokana na kukosa muongozo mzuri katika maisha yao pamoja
na shughuri zao za kimuziki.
"Msanii
atasikika na nyimbo zake jina litakuwa kubwa lakini matokeo yake wanaingia
katika matumizi ya madawa ya kulevya ni kwa sababu ya kukosa muongozo na
ushauli mzuri wa kuwaongoza katika maisha na kazi zake".
Ruge
aliongezea kuwa msanii mzuri ni lazima ume na kiongozi mzuri kwa ajili ya
kuongoza kazi zako pamoja na kuwa na mtu mzuri wa masoko ili uweze kufanya
vizuri kimasoko hususani kwa nia ya kufika kimataifa.
Credit to Pro24







0 comments:
Post a Comment