Msanii aliyejizolea
umaarufu mkubwa kutokana na style yake ya uigizaji Hussen Ramadhani Mkiete (27) aka
Sharomillionea amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari.
Akizungumza na Clouds
Fm Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Constatine Masawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo
kwa kusema msanii huyo alipata ajali hiyo majira ya saa mbili usiku maeneo ya
Maguzuni Songa karibu na Wilaya ya Muheza.
Alisema msanii huyo alikuwa njiani kwenda kumuona mama yake na alipata
ajali na gari aina ya Toyota Harrier lenye namba T478 BVR. Aidha alisema gari
hilo ghafla lilitoka nje ya barabara hatimaye kupinduka na kufariki dunia papo
hapo.
Hata hivyo RPC huyo alisema kuwa taarifa zaidi hazikuweza kupatikana kwa
kuwa msanii huyo alikuwa peke yake ndani ya gari hilo. Mwili wa marehemu
umehifadhiwa hospitali Teule ya Wilaya ya Muheza.
Hili ni pigo linguine tena kwa tasnia ya filamu nchini kwa kuangalia ni siku
chache tu kutokea kwa kifo cha Mlopela na hivi juzi tena kifo cha John Maganga
anaetarajiwa kuzikwa leo na hivi leo tena msanii Sharo milionea.
Samber Junior inatoa pole kwa familia ya marehemu, wasanii wote wa filamu na
muziki na watu wote walioguswa na msiba huu. Mungu ailaze Roho ya marehemu
Pema Peponi….Ameen.







0 comments:
Post a Comment