
MSANII wa muziki na filamu
bongo Baby Madaha,
amesema kuwa ngoma yake mpya ya ‘Nitenge’, inatarajia kuanza kusikika
leo kwani ameshaisambaza kwenye vituo vingi vya redio huku nyimbo hiyo
ikiwa inahusu mapenzi.
Msanii huyo alisema kuwa watu
wengi wamekuwa wakimuona kwenye filamu sana lakini safari hii nguvu zake
amezirudisha upya kwenye game la muziki ili kuwaonesha mashabiki wake kuwa
bado anafanya vizuri na wala hajapotea.
“Mimi huwa nafanya ngoma ambazo hazifi
ukisikiliza wimbo wangu wa ‘Amore’ hadi leo bado unafanya vizuri hivyo
hata huu mpya upo hivyo na nachopenda kuwaambia mashabiki wangu ni kwamba
nimekuja upya nikiwa na nguvu zaidi,” alisema.
0 comments:
Post a Comment