MSANII ambaye ni mama wa mtoto mmoja Sykner Ally au mama ‘Dillyfhaddy’ , amesema kuwa kwa sasa hawezi kufanya filamu hadi pale mtoto wake huyo atakapotimiza miaka miwili na kuendelea.
Skyner alisema kuwa kutofanya kwake filamu kumetokana na kauli ya baba wa mtoto, hivyo hata kwa upande ameona ni bora asitishe ili aweze kumlea vizuri mwanaye, kwani bado ni mdogo na hataki kuwa naye mbali.
“Baba wa mtoto ndio ameona bora nipumzike kufanya filamu kwa sasa ili niweze kumlea vizuri mwanangu maanake bado ni mdogo kwa hiyo sitaki kuwa nae mbali” alisema Skyner
Alisema akiendelea kufanya filamu kwa kipindi hiki anaweza kumfanya mtoto wake alelewe na mfanyakazi kitu ambacho hataki, hivyo atakapotimiza umri mkubwa kidogo ataendelea na kazi ya filamu.
0 comments:
Post a Comment