Mitandao ya kijamii ilikuaimejaa habari za rapa wa kike
kutoka Uganda zikisema kwa amekuwa chizi baada ya kuonekana akimkimbiza kibaka
wa laptop. Star huyo aliendelea kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa twitter
jinsi gani Uganda imekuwa si sehem salama kwake na kuna watu wanahatarisha
maisha yake.
watu ambao walitaka kufahamu zaidi kuhusu stori hiyo,
walijaribu kumpigia simu, lakini matokeo yake ilipokelewa na dereva wa boda
boda na hata alichokiongea kilionekana kutokuleta maaa yoyote.
kitendo hicho cha Keko, kimewalazimu baadhi ya watu
kuhitimisha kuwa amechizika. habari za hivi karibuni zinadai kuwa uchizi huo
stori ya Keko ulikuwa ni stunt tu, aliyoitumia kufanya utafiti kujua ni kiasi
gani anajulikana na watu
Keko ambae sasa yuko chini ya Sony Music Entertainment
ameahirisha uzinduzi wa album yake mara tatu sasa ambapo alitangaza kuizindua
mwezi wa nne tarehe 17 mpaka mwezi wa tano tarehe 4 na sasa kuipeleka mpaka
mwezi wa nane tarehe 10, na inasemekana Sony nao wanataraji kutangaza siku yao
ya kuzindua album hiyo.
Source: http://djfetty.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment