Saturday, August 4, 2012

ROMA APATA AJALI MBAYA AKIELEKEA KWENYE SHOW MOROGORO

Msaniii wa kizazi kipya kupitia hip hop ROMA amepata ajali mbaya barabara ya Morogoro. Roma anasema alikuwa yupo kwenye mwendo wa kawaida lakini ghafla tairi la mbele lilipata pancha na gari likaacha njia yake na kwenda kugongana uso kwa uso na fuso ambalo lilikuwa upande wa pili na gari hilo dogo alilokuwa akiendesha Roma kurudi lilipotokea.
Roma amesema ameelekea Hospital kwa check up zaidi ila aliokuwa nao kwenye gari hakuna aliyeumia wote ni wazima. 
Huyu ni mmoja kati ya marafiki wa Roma aliyekuwa nae kwenye gari wakielekea Morogoro kwenye show
Roma akitoa maelezo kwa askari wa usalama barabarani juu ya kilichotekea mpaka kusababisha ajali

Gari ya Roma ikiwa imeharibika vibaya

Source: http://djchoka.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment