Monday, August 27, 2012

MB DOGG KUGEUKIA MOVIE



BAADA ya kuwa kimya kwa muda mrefu katika muziki wa bongo fleva msanii Mbwana Mohamed ‘Mb Dog’ anatarajia kuonekana katika filamu mpya ya Nankonda wa Mikindani inayotarajia kuingia sokoni hivi karibuni.
Msemaji Mkuu wa kampuni ya usambazaji ya Dr. Cool Mzee Korongo alisema kuwa uwezo ulioonyeshwa na Mb Dog ndani ya filamu hiyo ni mkubwa sana na ni wazi kwa filamu hiyo, msanii huyo anatishia nafasi za wasanii waliopo katika sanaa ya filamu.
“Huyu kijana ameonysha uwezo mkubwa wa kupitiliza ndani ya hii movie ya Nankonda wa mikindani, yani kwa kiasi fulani anatishia nafasi za wasanii ambao tayari wako katika tasnia hii kwa siku nyingi” alisema Korongo.
Filamu hiyo ambayo Mb Dog ameigiza kama muhusika mkuu inatarajia kuingizwa sokoni hivi karibuni ikiwa inasambazwa na kampuni ya Dr. Cool Prodoction. Na itakuwa ni filamu ya kwanza kumtambulisha msanii huyo katika sanaa ya filamu.
“Filamu tayari imeshakamilika na ipo tayari kuingia dukani wakati wowote, na itasambazwa nchi nzima na kampuni ya Dr. Cool Production ambayo ndio watayarishaji wa filamu hiyo” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment