Sunday, April 15, 2012

AFANDE ATOA YA MOYONI



MSANI nguli wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele, amesema kuwa licha ya kutoaa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la  ‘Mashikolo Mageni’, lakini  mpaka sasa hakuna kituo kilichoupiga wimbo huo.cha kushangaza hakuna kituo hata kimoja kinachopiga kazi hiyo.

Msanii huyo alisema wimbo kuwa unahusu mambo mapya mapya, pia ukiwa na ujumbe mzito ndani yake lakini kinachomshangaza zaidi ni kwamba mpaka sasa hakuna kituo hata kimoja cha redio ambacho kimepiga wimbo huo.

Alidai kuwa watangazaji wengi wamekuwa wakimpigia simu na kumuomba rushwa ili wapige ngoma zake, ingwa kwa upande wake haoni kama ni sahihi wao kufanya hivyo.
“Yani mimi nashangaa sana hii nyimbo ni nzuri lakini hakuna hata redio moja ambayo imeshaupiga wimbo huu, na kuna baadhi ya watangazaji wananipigia simu wakinitaka niwape hela kusudi wagonge ngoma zangu” alisema Afande.
Aliongeza kuwa kingine ni kwa watangazaji hao kucheza nyimbo ambazo zinazotengenezwa na waandaaji wa jijini Dar es Salaam, wakati hata mikoani kuwa waandaaji wengi wazuri.

“kama umeshawahi kufanya uchunguzi ni kwamba hawa watangazaji wanakuwa wanapiga sana nyimbo ambazo zimetengezwa na maprodyuza wa hapa bongo wakati huko mikoani kuna maprodyuza wazuri sana” aliongeza.

0 comments:

Post a Comment